Kenya yafunga mipaka yake na Tanzania, Somalia

Fuente: https://www.voaswahili.com/a/kenya-yafunga-mipaka-yake-na-tanzania-somalia/5422612.html

Kenia cierra sus fronteras con Tanzania y Somalia

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, Jumamosi alitangaza kufungwa kwa mipaka kati ya nchi hiyo na majirani wake, Tanzania na Somalia, katika kile alichokiita "juhudi zaidi za kukabiliana na kuenea kwa virusi vya Corona."

El presidente de Kenia, Uhuru Kenyatta, anunció el sábado el cierre de la frontera entre el país y sus vecinos, Tanzania y Somalia, en lo que llamó "los mayores esfuerzos para frenar la propagación del Coronavirus".

kile alichokiita: construcción de relativo con referente "eso, el hecho", por defecto de clase 7 (KI), derivada de kuita: llamar; significa "lo que llamó..." Kati ya... na... es una construcción que significa "entre tal y tal sitio".

Katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja na vyombo vya habari kutoka Ikulu ya Nairobi, Kenyatta alisema ni marufuku kwa watu kutoka au kuingia Kenya kupitia mipaka hiyo. "Kuingia au kutoka nchini Kenya, ikiwa ni pamoja na magari ya abiria, sasa ni marufuku," alisema Kenyatta.

En un discurso lanzado directamente a los medios de comunicación desde la Casa Blanca de Nairobi, Kenyatta dijo que está prohibido que la gente saliera o entrara a Kenia a través de estas fronteras. "La entrada o salida desde Kenia, incluidos los automóviles de pasajeros, ahora está prohibida", dijo Kenyatta.

iliyorushwa es una construcción de participio para clase 9 (hotuba, discurso): "lanzado". Ikiwa es condicional de Kuwa con sujeto clase 9, con significado de "incluso si es el caso...".

Hata hivyo, rais huyo alisema magari ya mizigo bado yataendelea kuruhusiwa kuingia na kutoka "lakini ni lazima madereva wawe wamefanyiwa vipimo na kubaini kwamba hawana virusi vya Corona." Katika siku za karibuni serikali ya Kenya imesema kumekuwa na ongezeko kubwa la maambukizi kutokana na kutofuatwa kwa kanuni zilizowekwa kupambana na ugonjwa huo kwenye mipaka yanke na nchi jirani. Kenyatta anakitaja kuwa uingizaji wa maambukizi ya kiwango cha juu nchini mwake na hivyo basi kuwaweka raia wake katika hatari ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Sin embargo, el presidente dijo que aún seguirían estando permitidas la entrada y salida de los vagones de carga "pero es necesario que a los conductores les sean realizadas pruebas para comprobar que están libres del coronavirus". En los últimos tiempos, el gobierno de Kenia ha dicho que ha habido un aumento significativo en las infecciones debido al incumplimiento de las regulaciones establecidas para combatir la enfermedad tanto en las fronteras como en los países vecinos. Kenyatta lo denomina la introducción de infección más alta en su país y por tanto pone a sus ciudadanos en riesgo de infección por el coronavirus.

yataendelea kuruhusiwa: continuarán estando permitidas. wawe es subjuntuvo presente de KUWA 3ª p. pl. wamefanyiwa vipimo: "les sean realizadas pruebas". kutofuatwa es forma negativa de clase KU (14) del verbo KUFUATA: cumplir; se puede traducir como "incumplimiento". zilizowekwa es participio plural de kuweka: colocar. La construcción "kwenye... na..." significa "tanto en... como en..." anakitaja: "lo menciona"

Rais Kenyatta alieleza kuwa mipaka ya Kenya na nchi hizi mbili imeingiza maambukizi 43 ya virusi vya Corona ambayo ni robo ya visa 166 ilivyoripoti wiki jana na hivyo basi ipo haja ya dharura ya kuwazuia raia wa nchi hizo mbili kuingia mipaka yake. Aliongeza kuwa maambukizi 14 ni ya watu walioingia Kenya kupitia Wajir, 16 kupitia mpaka wa Namanga, 10 kupitia Mpaka wa Isebania, 2 kupitia mpaka wa Lunga Lunga na mmoja kupitia mpaka wa Loitokitok. Kenyatta vile vile alisema watu 78 waliopimwa na kupatikana na maambukizi ya virusi vya Corona kutoka nchi hizi mbili, wamerejeshwa nchini mwao kupata matibabu zaidi.

El presidente Kenyatta explicó que las fronteras de Kenia y esos dos países han importado 43 infecciones por el coronavirus, que es una cuarta parte de los 166 casos reportados la semana pasada y que existe una necesidad urgente de evitar que los ciudadanos de los dos países crucen sus fronteras. Agregó que las 14 infecciones son aquellas que ingresaron a Kenia a través de Wajir, 16 a través de la frontera de Namanga, 10 a través de la frontera de Isebania, 2 a través de la frontera de Lunga Lunga y una a través de la frontera de Loitokitok. Kenyatta también dijo que 78 personas que habían sido analizadas y se encontraron infectadas con el coronavirus en los dos países, han sido devueltos a su país para recibir tratamiento adicional.

ilivyoripoti es participio plural de kiripoti: reportar. ipo: hay, existe (con sujeto de clase 9: haya="necesidad"). haya ya dharura: necesidad urgente. wamerejeshwa: han sido devueltos.

Mpaka kati ya Kenya na Tanzania unapitia miji ya Namanga, Loitokitok, Taveta-Holili, Isebania na Lunga Lunga. Serikali ya Kenya imekuwa ikijikuna kichwa kutokana na maambukizi yanayoongezeka kila kuchao, huku visa kadhaa vikiripotiwa kutokea nchi jirani, hususan Tanzania na Somalia, na tayari imetangaza kuweka vituo vya maabara katika mpaka wake na Tanzania katika eneo la Namanga. Kenya inatarajia kupunguza maambukizi zaidi ya virusi vya Corona kupitia madereva wa malori ya masafa marefu nchini mwake na kuwahakikisha usalama wa raia wake. Baadhi ya madereva kwenye kituo cha mpaka kati ya Kenya na Tanzania, cha Namanga, wamekuwa wakilalamikia kile wanachokiita unyanyapaa. Kenyatta aidha alitangaza kuongezwa kwa muda wa marufuku ya kutoka nje usiku kote nchini, na zuio la kutoka au kuingia kwenye kaunti za Nairobi, Mombasa, Kwale, Kilifi na Mandera.

La frontera entre Kenia y Tanzania pasa por las ciudades de Namanga, Loitokitok, Taveta-Holili, Isebania y Lunga Lunga. El gobierno de Kenia se ha estado investigando el origen del aumento de infecciones cada año, con varios casos reportados de países vecinos, particularmente Tanzania y Somalia, y ya ha anunciado el establecimiento de centros de laboratorio en su frontera con Tanzania en la región de Namanga. Kenia espera reducir la transmisión del coronavirus a través de camioneros de alta velocidad en su país y garantizarles la seguridad a sus ciudadanos. Algunos conductores en la parada de la frontera entre Kenia y Tanzania, en Namanga, se han quejado de lo que llaman un estigma. Kenyatta anunció la extensión de la prohibición de los viajes nocturnos en todo el país, con el bloqueo de la salida o entrada a los condados de Nairobi, Mombasa, Kwale, Kilifi y Mandera.

imekuwa ikijikuna kichwa: textualmente "ha estado rascándose la cabeza" es una formación gerundiva muy coloquial que obviamente significa "ha estado investigando". imetangaza tiene como sujeto al Gobierno de Kenia, es un objeto. wamekuwa wakilalamikia: construcción gerundiva: han estado quejándose. kile wanachokiita: "lo que llaman..." kuongezwa kwa muda: aumento en el tiempo: prolongación, extensión.

VOCABULARIO

KUTANGAZA: ANUNCIAR, HACER SABER

KUKABILIANA: ENFRENTARSE, DETENER

KUENEA: AVANZAR, EXTENDERSE, DIFUNDIRSE

vyombo vya habari (8): Medios de comunicación

Ikulu: palacio presidencial Tanzano, Casa Blanca de Tanzania

makurufu (9): prohibición

KUPITIA: ATRAVESAR; CRUZAR

abiria (9/10): pasajero

gari la mizigo: vagón de carga

KUBAINI: DETECTAR, CERCIORARSE

karibuni: recientemente

ongezeko (9/10): aumento

kutokana: debido a, a causa de...

kufuata: respetar, seguir, cumplir

kutofuatwa: incumplimiento

kanuni (9/10): acuerdo, norma (canon)

kupambana: combatir

KUWEKA: PONER, COLOCAR

uingizaji (11/10): introducción, importación

kiwango( 7/8): nivel, estadio, fase

raia (9/10): ciudadano

KUELEZA: EXPLICAR

kisa, visa (7/8): historia, suceso, caso

KURIPOTI: INFORMAR, REPORTAR

haja (9/10): necesidad

haja ya dharura: necesidad urgente

dharura (9/10): confusión, agitación, urgencia

KUWAZUIA: IMPEDIR

zaidi (adj): adicional

Utibabu, matibabu (11/6): tratamiento médico

KUREJESHA: devolver, restaurar

KUREJESHWA: SER DEVUELTO

KUJIKUNA: RASCARSE

hususan: particularmente

masafa (6): rango, recorrido

lori, malori (5/6): camión

KUHAKIKISHA: GARANTIZAR

KULALAMIKA: QUEJARSE

unyanyapaa (11): estigma

aidha: además

zuio: bloqueo

kaunti: condado