Masifu ya asubuhi
Utenzi
Ee Mwokozi wa dunia wasaidie waokolewa wako nawe Mama wa Mungu utupatie ukombozi
14 NOVEMBA
SALA YA MWANZO
Ee Bwana, Usimamizi wa Bikira Maria Mama yetu
na maombezi ya Watakatifu wote wakarmeli
vitusaidie kufuata kiaminifu mifano yao
na kutumikia Kanisa yako
kwa maombi na kwa matendo.
Njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, Mwanao, anayeishi na kutawala nawe katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu daima na milele. Amina.
KUOMBEA DHABIHU
Ee Mungu Baba yetu, Utufanye tustahili kukutolea sadaka, na kwa mfano wa watakatifu wakarmeli, utuwezeshe tushuhudie nguvu ya uwepo wako, na tuonje mapema utamu wa utukufu wako, Kwa njia ya Kristo Bwana wetu.