Mnamo tarehe 2/11/2015 tulianza safari yetu alfajiri na mapema kutoka Bunju kuja Morogoro kwa ajili ya kuanza masomo ya Falsafa tukisindikizwa na mapadre wetu na hivyo idadi kuwa ya watu sita (6), Mapadre wawili Pd. Thomas Mtey na Pd. Victor Biramata, pia wanafunzi wapostulanti wane Athanas Ngasa, Pascal Dominic, Dickon Sambala na Deogratius Peter.Kwa kuwa hatuna nyumba ya malezi hapa Morogoro tulifikia katika nyumba ya shirika la Wamisionari wa Consolata, walitupokea vizuri na kuishi nao vyema ingawa kuna baadhi ya mambo hayakwenda sawa kiasi flani maana tulifika mahali ambapo ni mapya kwetu na hivyo kuzoea watu na mazingira ikachukuwa muda kidogo.
Jioni ya siku hiyo baada ya chakula kama jumuiya kwa pamoja walitukaribisha na tukajitambulisha kisha maisha kuendelea. Siku iliyofuata tuliendelea na usahili chuoni na hatiamaye kukamilisha taratibu zote na kuanza masomo. Pale Consolata tulikuta mambo mengi ambayo hatukuwa tukiyafanya katika jumuiya yetu ya Wakarmeli hasa kwa namna ya pekee social gathering kama utamaduni wao kila baada ya mwisho wa mwezi, na pia kusherekea kumbukumbu za kila mtu katika tarehe aliyozaliwa, hayo yoteyalikuwa mageni na mapya kwetu. Lakini tunamshukuru Mungu kwani tumejuwa mengi hasa katika kuishi maisha ya jumuiya na changamoto zake kwani tulikutana na kila aina ya mtu na tabia zake.
Mwisho kabisa tunawashukuru Mapadre wa Consolata tulioishi nao kwa mchango wao kwetu na zaidi wale wote waliokuwa wakituhudumia na zaidi uhusiano kati ya wanafunzi wa Consolata na sisi kwani umetujengea umoja na mshikamano wa kindugu, na pia kutokana na nje ya uwezo wetu basi baada ya mwaka wa kwanza wa masomo tuliweza kuhama Consolata na kupata nyumba nyingine ambapo tunaendelea na masomo ya chuo na malezi ya shirika pia.(Na Pascal Dominic)
HISTORIA FUPI YA MAANDALIZI YA KUHAMIA NYUMBA NYINGINE
Baad ya mwaka mmoja wa kuishi ndani ya jumuia ya wa CONSOLATA pale Cola- Morogoro huku tukisoma Falsafa, ilionekana kwamba kutakuwa na ufinyu wa nafasi kwakuwa kulikuwa na miito mingi ya vijana wa Consolata walio tarajia kujiunga, kwahiyo ilikuwa lazima tuhame. Jambo hili lilimpa changamoto mlezi wetu, hasa kuhusiana na mipango ya kufanikisha kupata makao mapya. Mnamo trh 24/07/2016, tulikuwa tumemaliza mwaka wa masomo na kuondoka ndani ya jumuia ya Consolata tukielekea Dar es Salaam. Hata hivyo baada ya wiki moja mbele tulipewa likizo ya wiki tatu kila mtu. Baada ya kurudi Mlezi wetu alitupatia Maelezo rasmi kwamba, pale Consolata tutahama na kwamba amepata nyumba nyingine maeneo ya Cola karibu na Chuo cha Jordani. Baada ya siku chache mbele tulifunga safari na kuenda kuangalia makao mapya. Tulifika mapema na kuona, kumbe makao yalikuwa rafiki hivyo tulifurahi na kurejea DSM ambapo tulianza kazi ya kufanya manunuzi ya vifaa vya ndani kama vile vitanda, vyombo, friji na vinginevyo. Tuliingia makao mapya trh 06/10/2016 kwaajili ya masomo ya mwaka wa pili. Hata hivyo tuliandamana na vijana wawili, Boniface na Felix, ambao walijiunga na shirika kwa safari ya wito. Ilikuwa ni Baraka kubwa kwakuwa ni dalili njema za ukuaji wa jumuia.
Changamoto
Huku tukiwa na furaha ya kuingia ndani ya makao mapya na mizigo yetu pamoja na mafundi wa kutufungia vifaa mhimu ndani ya nyumba, huzuni ilitukumba baada ya kugundua kuwa tulisahau mfuko wa vifaa vya umeme ambavyo fundi aliviandaa kwaajili ya kuja kufungia. Tulishindwa kupika ndani na hivyo tukalazimika kununua chakula hadi tulipo fanikiwa kufunga jiko kwa mda wakati vifaa vikifuatwa DSM. Hata hivyo baada ya wiki moja tulikuwa tumeshazoea kwa kiasi cha kuridhisha mazingira yetu mapya.
Mwisho
Tunamshukuru sana Mungu kwa maongozi yake ya upendo na busara, tunamshukuru mlezi wetu na shirika kwa ujumla, pamoja na watu wote wenye mapenzi meme. Mungu atubariki sote na kutujalia ustawi stahiki.(Na Dickson Sambala)
Historia Fupi kuhusu kuhama kutoka Seminari ya Allamano
Baada ya kukaa kwa takribani mwaka mmoja katika Seminari ya Mwenye Heri Allamano iliyochini ya shirika la wamisionari wa Maria Consolata Morogoro mnamo tarehe 25-07-2016 tuliaga na kuondoka katika Seminari hiyo mara baadaya kumaliza mihura ya masomo ya mwaka wa kwanza wa masomo ya falsafa.
Tunamshukuru Mungu kwa kila jambo alilotutendea kwa kipindi chote hiki katika historia ya shirika letu. Tunaishukuru jumuiya ya Mapadre wote wa Consolata ambao tulikaa nao katika nyumba hiyo, lakini wale pia ambao hatukuweza kukaa nao. Pamoja na hilo tunawashukuru waseminari wote tuliokaa pamoja nao kwa upendo na ushirikiano wao.
Tuliondoka katika Seminari ya Allamano tukiwa watatu yaani Athanas Ngassa, Dickson R. Sambala na Pascal M. Dominic pamoja na mlezi wetu. Tuliaga na kuondoka rasmi tarehe 25 ya mwezi julai nakuelekea Bunju, Dar es salaam na hii ilikuwa mara tu baada ya kumaliza mitihani ya muhura wa pili wa masomo ya falsafa kwa mwaka wa kwanza. (Na Athanas Ngassa)
HISTORIA FUPI YA MATALAJIO YETU
Jumuiya ya karmeri katika jimbo la Morogoro tunamatarajio kadhaa katika kustawisha kiroho na kimwili kwa wanajumui wote na jamii yeto inayo tuzunguka.
Baadhi ya matarajio yetu ya katika jimbo la morogoro ni kama ituatavyo:
>Tunategemea kujenga nyumba ya malezi kwa ajili ya wanafunzi wa jumuiya ya karmeli.
>Tunategemea kutoa huduma kwa jamii inayotuzunguka kiroho na kimwili.
>Tunategemea kujishughurisha na kazi ndogo ndogo za uzalisha mali mfano ufugaji,kilimo n.k
>Kujifunza kwa kina namna ya kusali kuishi kindugu pamoja na kutafakari ili tuweze kuishi kulingana na matakwa ya Yesu kristo.
>Tunategemea kujifunza namna ya kutoa huduma mbalimbali za kanisa pamoja na kutoa huduma mbali kwa jamii nzima inayotuzunguka. (Na Felix Damas)