Sura ya 19
Nanyi ndugu wengine pia, shika mbele yakoo kwa heshima ya unyenyekevu, nia yako sio kwake ila kwa Kristo aliyemweka yeye juu yako na huyo kwa wale ambao wanayaongoza makanisa. Alisistiza maneno haya; yeyote atakayewasikilizeni amenisikiliza mimi na yeyote atakayewakosea heshima amenikosea mimi. Kama ukibaki na nia hiyo hutaonekana kuwa na hatia ya kudharauliwa, lakini utafurahia uzima wa milele kama tuzo ya utii wako.
Sura ya 20
Hapa kuna mambo machache nimeyaandika chini ili kuwapatia mwongozo wa namna ya kuishi. Lakini Bwana wetu katika ujio wake wa pili, atawapatia tuzo yule ambaye amefanya zaidi ya kinachotakiwa. Angalia kuwa mipaka ya akili ya kawaida haizidi, hatahivyo akili ya kawaida ni mwongozo wa wema.