Mwisho wa maisha haya tutahukumiwa juu ya upendo (Yohana wa Msalaba)
KAULI MBIO YA SHIRIKA
Zelo Zelatus Sum pro Domino Deo exercituum
Nimejawa wivu mwingi kwa ajili ya Bwana, Mungu wa majeshi (1Fal 19:10)
Padre Alfredo Mkuu wa Komisarieti ya La Bruna
Kanisa la Karmeli la Makao Makuu ya Komisarieti yetu ya La Bruna Napoli Italia
Shirika la wakarmeli lilianzia katika mlima Karmeli ulioko kule Israele (Palestina). Ampapo Alberto Avogadro, Patriarka wa Yerusalemu kati ya mwaka 1206 na 1214 aliwapatia wamonaki wa kilatini waliokuwa wakiishi Mlima Karmeli kanuni ya maisha (formula vitae). Kanuni hii ilikubaliwa na Papa Onorio III tarehe 30.1.1226, halafu tena ikaidhinishwa na Papa Gregori IX tarehe 6.4.1229 na tena ikaidhinishwa na Papa Innocent IV tarehe 8.6.1245. Papa huyu wa mwisho hatimaye aliipitisha kanuni hiyo tarehe 1.10.1247 kwa sherehe kuwa kanuni ya kudumu ya shirika la kitawa la Wakarmeli. Kwa kupitishwa kanuni hiyo wamonaki walianza kutambulikana kuwa ni watawa rasmi. Baada ya hapo shirika limeendelea kukua na kusambaa sehemmu mbalimbali duniani
Karmeli katika Afrika imeenea katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zimbabwe, Burkina Faso, Cameroon, Kenya, Mozambiki, na Tanzania.
Shirika la wakarmeli (O.Carm) limekuwepo Tanzania tangu mwaka 2009. Juhudi za kuanzisha shirika la karmeli nchini Tanzania zilianza toka mwaka 1988. Vijana wa kitanzania walikwenda kusoma na kufanya malezi Italia. Baada ya kipindi cha masomo walianzisha rasmi misheni tarehe 1.10.2009 huko Bunju "A". Konventi ilibarikiwa tarehe 8.10.2009 na Mhashamu Askofu Methodius Kilaini, aliyekuwa askofu msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Mapadre wakarmeli wanafanya kazi katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam katika Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli iliyotangazwa parokia tarehe 24.8.2012 wakati wa upadrisho wa Padre Dominic John Somola.
JINA LA SHIRIKA
Ordinis Fratrum Beatissimae Virginis Mariae de Monte Carmelo -Latin - Ordinis Carmelitarum (O.Carm): Ufupisho wake: Order of Carmelites (O.Carm.)
Shirika la Ndugu wa Mwenye Heri sana Bikira Maria wa mlima Karmeli