Nyumba yetu ya Morogoro
Baada ya maisha ya kupanga tangu mwaka 2015 hatimaye Mwaka wa 2019 ulikuwa mwaka wa hatua mpya katika maisha yetu ya Wakarmeli na ya Komisarieti kwa ujumla baada ya kupata makazi ya kudumu. Huu ndio mwaka ambao Viongozi wetu walikubali kununua nyumba ya malezi hapa morogoro. Mwanzo tulikuwa wapangaji kwa muda wa miaka 5, tangu mwaka 2015 tuliokaa pale Consolata Seminary na tangu mwaka 2016 tukawa wapangaji kwa Mr. Godfrey Machumu. Baada ya kuona kuwa iko karibu sana na Chuo cha Jordan ambako ndiko wanakosoma, tulimwomba mwenye nyumba aweze kutuuzia nyumba yake. Mwanzoni alikataa. Lakini baadae alikubali na tukawaomba wakubwa zetu nao wakakubali hatimaye tukainunua. Ilikuwa ni tarehe 12 Disemba 2019 ambapo Komisario alitoa taarifa kuwa watatuma fedha kwa ajili ya ununuzi wa nyumba. Ilikuwa siku ya furaha sana. Malipo yalikamilika mwezi 4 mwaka 2020. Safari hii ilihitaji sala na majitoleo mengi sana, nakumbuka vijana wanaolelewa walikuwa wakiomba kila siku ili tuweze kufanikiwa katika mpango huo na kweli Mungu alisikiliza sala zetu tukafanikiwa. Na kwa msaada wa sala za Bikira Maria tukafanikiwa. Tunamshukuru sana Mungu kwa wema wake aliotutendea. Kwa sasa kunafanyika juhudi ili tuweze kuongeza vyumba vipya.
Casa Carmelitana Morogoro
Dopo una vita di pianificazione dal 2015, finalmente il 2019 è stato l'anno di una nuova pietra miliare per i Carmelitani della Tanzania e anche il Commissariato generale della Bruna. Era l'anno della decisione di avere residenza permanente. Questo è l'anno in cui i nostri leader hanno deciso di acquistare una casa di formazione qui a Morogoro. Inizialmente eravamo inquilini per 5 anni, a partire dal 2015 al Seminario della Consolata e dal 2016 diventando inquilini del signor Godfrey Machumu. Dopo aver visto che era molto vicino al Jordan College dove studiano i nostri studenti, abbiamo chiesto al proprietario di venderci la sua casa. All'inizio ha rifiutato. Ma più tardi ha accettato e abbiamo chiesto ai nostri superiori e hanno anche concordato. Era il 12 dicembre 2019 che il Commissario Generale annunciò che avrebbero inviato il bonifico per l'acquisto della casa. È stata una giornata molto felice. Siamo riusciti a pagare tutti i soldi al proprietario entro aprile 2020. Pregavamo ogni giorno nella nostra comunità per questo scopo. Ricordo che gli studenti pregavano ogni giorno con la fede che avremmo avuto successo ed è davvero Dio ci assaudito e ci ha concesso l'abitazione. Crediamo che le preghiere della Vergine Maria abbiano contribuito al successo. Siamo molto grati a Dio per la sua bontà nei nostri confronti. Attualmente si sta compiendo uno sforzo per aggiungere nuove stanze.