Alijiunga na Shirika la Wakarmeli 18.08.2022. Kwa sasa anasoma Filosofia katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Jordan Morogoro
FAMILIA.
Kwanza kabisa namshukuru Mungu kwa yote aliyo nijalia,na anayoendelea kunitendea, pia nawashukuru watu wote tunao ishi nao kama wanajamii katika safari ya maisha ya hapa duniani.
Kwa jina naitwa KASIANO DIDAS SOKONI, nilizaliwa Jimbo Katoliki la Sumbawanga, Parokia ya Chala, kigango cha Kantawa, jumuiya ya mtakatifu Yohane mbatizaji mnamo tarehe 08/08/2001, Ambapo mimi ni mtoto wa tatu katika familiya ya watato kumi na moja kotoka kwa wazazi wetu, DIDAS SALVATORY SOKONI na GRACE EGIDIUS KISATO wote wakiwa wamezaliwa mkoa wa Rukwa, Jimbo Katoliki la Sumbawanga.
ELIMU.
Nikiwa mtoto wa miaka nane baada ya kuzaliwa nilianza kusoma elimu ya shule ya msingi mwaka 2008 kutoka katika shule ya msingi Kantawa iliyopo mkoani Rukwa, Ambapo elimu ya msingi nilidumu kwa muda wa miaka saba na kuhitimu mwaka 2014 katika shule hiyohiyo .Kwa nguvu za Mungu nilifanikiwa kufaulu na bada ya hapo nilijiunga na elimu ya Sekondari katika Seminari ndogo ya MT.YOHANE PAULO II au ST.JOHN PAUL II SEMINARY mwaka 2015 iliyopo mkoa wa Katavi kwaajili ya kozi fupi yaani, pre form one iliyodumu kwa mwaka mmoja, mwaka mmoja baadae 2016 nilianza masomo rasmi ya sekondari mpaka kuhitimu kidato cha nne mwaka 2019 katika seminari hiyohiyo. Napo Mungu hakuweza kuniacha, nilifaulu kwenda kidato cha tano. Nilichaguliwa kujiunga na shule ya NKASI HIGH SCHOOL iliyopo mkoani Rukwa. Kuanzia mwaka 2020 na kumaliza 2022, na kwa neema yake Mungu nilifanikiwa kufaulu.
WITO.
Safari ya wito au hamu ya kutaka kumtumikia Mungu ilianza nikiwa shule ya msingi, Baada ya mjomba wangu kupata daraja takatifu ya upadre mwaka 2013 nikiwa dalasa la sita, tangu hiyo hamu kuniijia niliweza kuwaeleza wazazi wangu hamu ya moyo yangu, wazazi wangu waliridhia ombi hilo, Baada ya kuridhia ndipo walipo amua kunitafutia seminari ndogo na walifanikiwa kupata seminari ya MT. Yohane paulo II, ambako huko nilisoma miaka mitano kwa maisha ya huko niliyapenda kutokana na maisha ya Sala na elimu nzuri juu ya Mungu iliyo nifanya kuendelea kuongeza hamu na tamaa ya kuwa padre ,nikiwa advance nilikutana na mtu mwenye elimu juu ya upadre na juu ya mashirika, na aliweza kuelezea na kufafanua kwa undani juu ya upadre wa jimbo na wa shirika, Baada ya kutoa elimu hiyo juu ya upadre na mashirika ,nilijikuta nimevutiwa na shirika la wakarmeli kutokana na karama zake za Sala,Tafakari na Maisha ya huduma kwa watu, nilimfuata na kumwelezea juu yangu na hivyo aliweza kutafuta namba za mkurugenzi wa miito nikaongea nae, naye aliweza kunipa maelekezo juu ya maisha ya Shirika. Mnamo tarehe 18/08/2022 ndipo nilipoanza safari ya Utawa katika Shirika la Wakarmeli bunju. Na sasa nimemaliza mwaka mmoja wa Aspirant najianda kuanza Falsafa katika Chuo kikuu cha Jordan- Morogoro.