Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli bunju leo 18 Juni 2017 imeadhimisha sherehe ya Mwili na Damu Takatifu ya Bwana wetu Yesu Kristo, kwa watoto 229 kupata Komunyo ya kwanza baada ya maandalizi. Ilikuwa ni furaha kubwa kuona watoto hawa wakiijongea meza ya Bwana. Misa hiyo imeongozwa na Paroko padre Thomas Mtey, O.Carm. Baada ya Misa Takatifu yalifuata maandamano yaliyozunguka katika viunga vya parokia hiyo. Watoto hawa wametoka katika vigango vya Kinondo, Vikawe, Kidimu na Mabwepande. Kwaya iliyoimba katika Misa hiyo ni kwaya ya Mt. Joseph.