Kristo ndio mwisho wa matatizo.
Kifo kinachokuja mtu akiwa ndani ya Kristo, basi kifo kinakuwa ni safari ya kumwendea Yesu na kuingia katika uzima wa milele. Kinachotokea katika maisha tunajaribu kuelewa maana yake. Injili tuliyosoma ni sehemu ya Injili inayoeleza jinsi Mitume na watu wengine walivyokula mkate lakini hawakuelewa. Hawakuelewa mkate ulimaanisha nini. Mkate ni ishara ya kitu kingine zaidi. Kitu hicho kinadumu milele, yaani huruma au rehema na upendo. Chanzo au chemchemi ya huu mkate wa uzima ni upendo usio na kikomo na unaodumu milele. Upendo huu umeumba mbingu, umetengeneza historia ya mwanadamu na Mungu. Upendo huu ndio unaotoa chakula kwa kila kiumbe. Kumbe basi historia nzima ya maisha na uumbaji wote ni kama kitabu. Kitabu hiki ni lazima kisomwe. Kisipo somwa ujumbe hautafika kwetu. Mwanadamu anaposhindwa kuelewa maana ya maisha huyaharibu lakini anapoyaelewa huyatunza. Tunaamini ndugu zetu walielewa maisha wakayatunza kwa kupata chakula cha uzima. Mkate ni alama ya maisha. Zamani walitumia alama mbili za umama maji na upepo. Sasa mkate ni alama ya ubaba. Mkate maana yake ni nini? Kuna somo la fumbo. Uumbaji wote ni fumbo la Mungu. Tufikirie mkate wa Ekaristi..hili ni fumbo. Tusipoelewa fumbo lililomo ndani basi hapa kuna shida. Kanisa linatamka maneno ya msamaha. Kanisa limepewa mamlaka ya kufunga na kufungua.
Hebu sali hii sala nzuri sana.
Hii sala husaliwa wakati wa kuwapa wagongwa Mpako Mtakatifu.
Ondoka, roho ya kikristo, kutoka ulimwengu huu,
kwa jina la Mungu Baba Mwenyezi aliyekuumba,
kwa jina la Yesu Kristo,
Mwana wa Mungu aliye hai,
aliyekufa msalabani kwa ajili yako,
kwa jina la Roho Mtakatifu aliyemiminwa ndani yako.
Chukua nafasi yako leo kwa amani,
na uyaweke makao pamoja na Mungu ndani ya Sayuni takatifu,
pamoja na Mtakatifu Yosefu,
malaika na watakatifu wote wa Mungu...
Urudi kwa Muumba wako aliyekutengeneza kutoka vumbi za dunia.
Wewe ambaye roho yako itatoka mwilini mwako,
Maria Mtakatifu, malaika na watakatifu wote waje kukulaki...
Nawe ujaliwe kumwona Mkombozi wako uso kwa uso....
Walio purgatorio wamekufa katika neema na urafiki na Mungu. Lakini hawajatakaswa kikamilifu. Lakini hawa wana uhakika na wokovu wa milele baada ya kufa wanatakaswa ili wawe na hali kamili ya kumwona Mungu.
Kumbukeni kuna Kanisa moja lakini liko katika hatua tatu. Kanisa lililo vuka, yaani, Kanisa la mbinguni, Kanisa linalosafiri, Kanisa linalotakaswa -Kanisa lililoko toharani-Purgatorio Kazi ya mtu ikiteketea, atapata hasara; ila yeye mwenyewe ataokolewa; lakini ni kama kwa moto (1Kor 3:14) -. Sisi wote tumeunganishwa na Upendo wa Kristo.
Kuhusu kusamehewa katika ulimwengu ujao soma Injili kadiri ya Mathayo
Naye mtu yeyote atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakayenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ujao (Mt 12:32).