Shirika la wakarmeli asili yake ni Mlima Karmeli, ulioko Palestina, ambao, kama tunavyosoma katikaKitabu cha II cha Wafalme, nabii Elia mkubwa alitetea imani ya kweli ya Mungu wa Israeli, na kushindachangamoto zilizotoka kwa makuhani wa Baali. Ilikuwa pia katika mlima ule wa mlima Karmeli ambapo nabii yule, aliomba katika upweke, na hatimaye aliona wingu dogo ambalo lilileta maisha kwa kutoa mvua baada ya ukame wa muda mrefu. Tokeapo, mlima huu umekuwa kuchukuliwa kuwa bustani ya Palestina na ishara ya uzazi na uzuri wa aina yake. Kwa kweli, "Karmeli" maana yake "bustani".Katika karne ya XII (labda baada ya kampeni ya tatu ya vita vya mslaba, 1189-1191), baadhi ya wafanya toba -mahujaji waliokuwa wametoka Ulaya, walikusanyika pamoja karibu na "chemchem ya Elia", katika moja ya mabonde mmbamba ya Mlima Karmeli. Walitaka kuishi ukristo wao waeremiti (hermits)wakiiga mfano wa nabii Elia katika nchi ya Bwana wetu Yesu Kristo. Eliya anachukuliwa kama mwanzilishi na baba wa umonaki. Wakarmeli walibakia wafuasi waaminifu wa Eliya ambaye ana uhusiano na Mlima Karmeli kupitia matukio ya Biblia. Katikati ya vyumba vyao kulijengwa kanisa ambalo walijitolea kwa Bikira Maria walilijenga kwa heshima yake, Mama wa Yesu, hivyo kuendeleza hisia ya kuwa Maria ni Mama yetu kama Mama wa mahali na kama mlezi, na wao kujulikana kwa jina lake:
Wakarmeli Watanzania — May 28, 2017 3:06:09 PM