Roho ya Wakarmeli ni hamu kubwa na ya ndani ya kutaka kuwa na uzoefu wa moja kwa moja wa Mungu. Kwa maneno mengine, roho ya Wakarmeli i katikati ya maombi ya moyo, yanayoeleweka kama urafiki wa upendo kati ya nafsi ya mtu na Mungu, na kutafakari kama zawadi ya bure ya Mungu. Hivyo, roho ya Wakarmeli inalenga kukuza uhusino makini wa mtu na Yesu Kristo kwa njia ya sala.
Sources of Carmelite Spirituality/Vyanzo vya Roho ya Wakarmeli
Roho ya Wakarmeli
Kukutana na Mungu rohoni
Roho ya Wakarmeli ni hamu moto moto ya nafsi ya kutaka kuwa na uzoefu wa moja kwa moja wa Mungu, kukutana naye rohoni . Kwa maneno mengine, roho ya Wakarmeli i katikati ya roho wa maombi, inayoeleweka kama urafiki wa upendo kati ya nafsi ya mtu na Mungu. Mtu hujizamisha katika tafakari kama zawadi ya bure ya Mungu. Roho ya Wakarmeli inalenga kukuza uhusino makini kati ya mtu na Yesu Kristo. Huu ndio mvuto ambao Wakarmeli wameuona na kuutamani kwa Bikira Maria na nabii Eliya. Hawa wawili walikutana na Mungu rohoni mwao, katika upweke sala na utii sikivu wa sauti ya Mungu.
Vyanzo vikuu ya Roho ya Wakarmeli (Carmelite Spirituality):
Ili kukua kiroho na kuingia katika mabadiliko ya utakatifu Wakarmeli maisha yao ya kiroho yanakuzwa na vyanzo:
Vilivyoandikwa:
Kanuni ya Shirika, (Kanuni ya Mt Albert wa Yerusalemu)
Katiba za Shirika.
Biblia Takataifu
Mafundisho ya Mababa wa Kanisa
Maandishi ya kiroho ya Watakatifu Wakarmeli kama vile:
Teresa wa Avila
Yohane wa Msalaba
Teresa wa Lisiuex (wa mtoto Yesu),
Pamoja na Watakatifu wengine Wakarmeli.
Visivyoandikwa
Maisha ya Bikira Maria
Maisha ya Mtakatifu nabii Elia