SAFARI YANGU NA GABRIEL. G. MJORA.
Kwa majina naitwa Gabriel Godfrey Mjora, nimezaliwa katika jimbo katoriki la msoma, parokia ya mt. mikael malaika mkuu sirari mkoani mara.
Baba yangu anaitwa Godfrey Mjora kutoka kabila la wazanaki na mama yangu anaitwa Lucia joseph kutoka katika kabila la wakurya.
Mimi ni mzaliwa wa kwanza kati ya watoto tisa ambapo tulizaliwa mapacha, mimi kama Kurwa na mwenzangu kama Dotto, ambapo tulizaliwa tarehe 26. 04. 2001 katika kijiji cha buriba kata ya sirari wilayani tarime. Nilipokea sakramenti ya ubatizo na komunio takatifu tarehe. 23. 12. 2018 chini ya Fr. Alex Kamugisha katika parokia ya Mt. Mikael Sirari. Mnamo tarehe 31. 05. 2026 nilipokea sakramenti ya kipaimara katika parokia ya Bikira Maria wa Mlima karmeli Bunju chini ya Muhashamu Askofu Stephan Msomba.
ELIMU
Nilianza shule ya msingi mwaka 2008 katika shule ya msingi keryoba wilayani tarime, ilipofika mwaka 2011, wazazi wakaafikiana kuturudisha darasa la kwanza wakidai kwamba uwezo wetu bado upo chini. Mwaka 2018 nilijiunga na shule ya sekondari sirari iliyopo mkoani mara, nilifanikiwa kuhitimu kidato cha nne mwaka 2021 na kupata ufaulu uliyo niwezesha kuendelea na elimu ya advance. Mwaka 2022 nilijiunga na shule ya sekondari Ngudu kwa ajili ya kuendelea na elimu ya kidato cha tano na sita.
WITO
Safari yangu ya wito ilianza tangu nikiwa darasa la kwanza baada ya kuvuvitwa na ibada ya kuabudu ekaristi takatifu ilivyo kuwa ikiendeshwa na paroko parokia ya sirari, padre erenest kamgisha, nilikuwa nikivutiwa sana nikiona namna yesu wa ekarist akiinuliwa juu ndani ya monstras takatifu na namna padre alivyokua akiongoza misa kwa takatifu kwa kuimba hasa katika ritrujia ya ekaaristi takatifu. Tendo hilo lilinivutia nakunifanya nitamani siku moja kuja kuwa miongoni mwa waadhimishaji wa misa takatifu.
Wito huo uliendelea kukua ndani mwangu. Lakini baada ya kuingia shule ya secondary, wito huo ulianza kufifia kutokana na hatua mbalimbali za ukuuaji. Nilipofika kidato cha nne nilianza kutamani tena kuendeleza wito wangu baada ya kupitia changamoto nyingi katika masomo, ndipo nilipo amua kuendeleza na kukuza wito ndani yangu Zaidi. Nilifanikiwa kuwa kiongozi wa ritrujia katika shule ya secondary ngudu nikiwa kidato cha tano. Nilishilikiana na viongozi wenzangu vizuri na kusababisha kuamsha Imani ya wakristo katika shule. Pamoja na mafanikio mengi sana tuliyopata tulikua tukitiana nguvu na kufundishana kuhusu wito mtakatifu wa utawa.
Kwa mara ya kwanza nilikua nikifikiria kujiunga na shirika la wabenedictini mimi na wenzangu wawili lakini kabla sijaamua, niliaamua kujaribu kufuatilia shirika jingine ambapo nilijaribu kumuulizia sister angel kuhusiana na shirika lao la kikarmel kwani nilikuwa nimevutiwa na maisha yake aliyokua nayo ya upendo na undugu. Alinielezea juu ya karama ya shirika na kujikuta navutiwa nalo. Niliamua kuandika barua ya kuomba kujiunga na shirika la wakarmel kwa mara ya kwanza tar. 08. 12. 2023. Sister alinipatia namba ya simu ya frt. Gabriel Mutiti. O. carm ambae alinipa mwongozo na kuniambia nitulie kwanza mpaka nikimaliza mitihani ya kidato cha sita ndipo nitakapo pewa mjibu ya barua yangu.
Namshukuru mungu baada ya kumaliza kidato cha sita frt Gbriel alipatia namba ya mkurugenzi wa miito Fr. Victor Biramata. O. carm. Nilifanikiwa kuongea nae kwa mara ya kwanza ambapo aliniambia kwamba kwa mwaku huo hawachukuio vijana. Sikukata tamaa niliendelea kumuomba mungu huku nikifanya mpango wa kujiunga na shirika la visent wa paul. Katika harakati za kuangaika kutafuta shirika, namshukuru mungu sister Angel alinipigia simu na kuniambia kwamba nahitajika katika shirika la wakarmel kwa ajili ya mazungumzo. Nilifurahi sana na kumshukuru mungu.
Niliingia katiaka shirika la wakarmel tar. 26. 07. 2024 mda wa saa 7:11. Mchana katika nyumba iliyopo bunju dar-es-salam. nilipokelewa vizuri na frt. Gabriel Mutiti kasha kunitambulishwa kwa mapadre na mafrater wote wakarmeli. Jumuiya yote ilinipokea kwa upoendo na furaha. Ilipofika mida ya saa 3:24 usiku alinikutanisha na mkuu wa nyumba padre Dominic Somola. Naye alinipokea kwa furaha na kuniruhusu niendelee kuishi ndani ya karmel na kuanza malezi. Nilifanikiwa kufanya malezi kwa kipindi cha mwaka mmoja, na tarehe 02. 10. 2025 nilipokelewa kwa furaha na Padre Victor Biramata katika nyumba ya malezi iliyopo morogoro kwa ajili ya kuendelea na malezi na masomo katika ngazi ya falsafa.
MASOMO YA FALSAFA
Ninamshukuru Mungu nilianza rasmi masomo ya falisafa mnamo tarehe 24. 11. 2025 katika chuo kikuu cha Jordan kwa mwaka wa Kwanza. Licha ya kuwa na mwanzo mgumu Katika mazingira mapya ya chuo, nilianza kupata uzoefu mdogomdogo wa kitaalauma katika chuo hicho na uzoefu wa Ritrujia, huduma kwa watu, sala na utume katika nyumba ya malezi morogoro chini ya uongozi wa Padre Victor Biramata Jambo lililonisaidia kuweza kukuza na kuendeleza karama zilizomo ndani Yangu katika kumtumikia Mungu. Mnamo tarehe 07. 08. 2026 nilimaliza masomo ya falisafa ya Kwanza
BIKIRA MARIA WA MLIMA KARMELI.....UTUOMBEE.