Tarehe 03.08.2019 Shirika la Wakarmeli nchini Tanzania, limeandika historia baada ya vijana watatu wa kwanza waliolelewa Tanzania kuweka nadhiri zao za muda katika Makao Makuu ya Shirika yaliyoko bunju katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Vijana hao ni frt. Dickson Richard Sambala, frt. Pascal Dominic Mkaka, na frt. Athanas Mhina Ngassa. Askofu Mkuu mtaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo ndiye aliye adhimisha Misa hiyo.
Baada ya kuingia Karmeli mwaka 2014, walisoma falsafa pale JUCO na kupata shahada ya falsafa mwaka 2018. Wakaingia unovisi mwaka 2018.