Naitwa John Kheri Madava Mzaliwa wa jimbo katoliki la Moshi Parokia ya Mtakatifu Yohane Mtume ,ni mzaliwa wa kwanza kati ya watoto watatu wa mama Cecilia Baltazari Mrema ,nilizaliwa mwaka 09/02/1994 Mkoani Morogoro ,mama yangu kwa kabila ni Mchagga tokea Moshi Kilimanjaro na baba yangu ni Msambaa kutokea Lushoto Tanga sikubahatika kupata historia yake kwa undani kwasababu alifariki nikiwa bado na umri mdogo,hivyo nililelewa na bibi mzaa mama ,mama mzazi pamoja na baba wakufikia.Nilibatizwa mnamo tarehe 09/09/1995 katika parokia ya Mt.Yohani mtume kirua Iwa huko moshi Kilimanjaro.
Familia yangu ina jumla ya watoto watatu ,wa kwanza nikiwa ni mimi John Kheri Madava mtoto wa baba Kheri Madava ambaye kwa sasa ni marehemu,baada ya baba kufariki mama aliolewa na baba mwingine na nikabahatika kupata wadogo zangu wawili Jackline Monyo na Erick Monyo ambao hawa kwa dini ni walutheri kwasababu baba yao ni wa dini hiyo.
ELIMU
Kwa upande wa elimu nilianza darasa la kwanza katika shule ya msingi Iwa iliyopo Moshi mkoani Kilimanjaro mwaka 2001 hadi mwaka 2007 nilipohitimu nakuchaguliwa kujiunga na shule ya secondari ya Pakula iliyopo Moshi Kilimanjaro kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2011 nilipohitimu kidato cha nne,baada ya masomo hayo ya secondari nilijiunga na chuo kikuu cha Tumaini Makumira mwaka 2013 hadi mwaka 2014 kwa kozi ya cheti cha sheria na mwaka 2014 hadi 2016 kwa ngazi ya Diploma ya sheria baada ya hapo nilibahatika kuchaguliwa kujiunga na chuo kikuu Mzumbe tawi la Mbeya mwaka 2016 hadi 2019 ambapo nilihitimu nakupata shahada ya kwanza ya sheria (Bachelour in Laws(L.L.B) which means Latina Legum Baccalaureus).
WITO
Wito wangu nilianza kuutambua tangu nikiwa mdogo na ilikuwa ni tamanio langu kuwa padre,tangu nikiwa mtoto mdogo wazazi na watu wengine walipenda kuniita “baba paroko”sikujua nini kilikuwa kinawasukuma kuniita hivyo,nilipofika darasa la nne nilijiunga na shirika la Mt.Aloisi Gonzaga ambalo lilihusika na malezi ya watumishi wa Altareni ,nilikuwa nikifurahishwa kwa namna mapadre walivyokuwa wakiendesha ibada na walivyokuwa wakitoa huduma kwa jamii nilitamani siku moja kuwa kama wao.baada yakumaliza darasa la saba nilibahatika kupata nafasi yakujiunga na seminari ya Uru lakini haikuwezekana kutokana na sababu za kiuchumi kwa wakati ule.mbali na yote hayo sikukataa tamaa niliendelea kumtumainia Mungu nakumwomba aniongoze ili niweze kufikia kile nilichokuwa nakitamani ndani mwangu ndoto ya kuwa padre.
Kwa upande wa shirika hili la Bikira Maria wa mlima Karmeli lilikuwa ni geni kwangu,nililifahamu shirika hili kupitia kwa dada yangu ,sista Germana Tarimo ambaye naye ni sister katika shirika hili ,yeye alinielezea kuhusu shirika karama ya shirika na mahali linapopatikana ,pia alinisaidia kupata mawasiliano na mkurugenzi wa miito wa shirika padre Victor Biramata (O.cam) ambaye nilibahatika kukutana naye na akanipa maelekezo na ushauri kuhusu shirika hili nilivutiwa nalo na nikachukua maaumizi yakujiunga nao.japokuwa nimeyafahamu mashirika mengi lakini shirika hili limekuwa mahali bora kwa mimi kuwepo.
Tarehe 09/09/2020 tarehe iliyofanana na tarehe na mwezi niliyobatizwa (09/09/1995) ndio tarehe niliyo ripoti katika nyumba ya malezi Bunju,nilipokelewa kwa furaha na padre Dominiki somola (O.carm),nayafurahia maisha haya ya wito ,ilikuwa ni matamanio yangu kuishi maisha yakumpendeza Mungu na kuishi maisha ya pamoja namshukuru Mungu kwa zawadi hii ya wito namwomba kile alichokianzisha ndani mwangu akapate kukikamilisha..