Ufafanuzi wake
Roho ya wakarmeli inajipambanua kwa kwa njia ya sala, tafakari, ukimya, kujiachilia kwa nafsi na kuwa na hamu kubwa ya kufanya maendeleo ya kiroho yanayo mwezesha mtu kuwa na muungano wa ndani na Mungu. Hivyo Roho ya Wakarmeli ni Kukutana na Mungu rohoni. Hiyo ndiyo hamu moto moto ya nafsi ya kutaka kuwa na uzoefu wa moja kwa moja wa Mungu, kukutana naye rohoni . Kwa maneno mengine, roho ya Wakarmeli i katikati ya roho wa maombi, anayeeleweka kama rafiki wa upendo kati ya nafsi ya mtu na Mungu, ambaye hujizamisha katika tafakari kama zawadi ya bure ya Mungu. Roho ya Wakarmeli inalenga kukuza uhusino makini kati ya mtu na Yesu Kristo. Huu ndio mvuto ambao Wakarmeli wameuona na kuutamani kwa Bikira Maria na nabii Eliya. Hawa wawili walikutana na Mungu rohoni mwao, katika upweke na utii wa sauti ya Mungu.Chanzo chake ni Maisha ya Maria na nabii Eliya, Kanuni ya shirika na maandishi ya watakatifu.
Vilivyoandikwa:
Kanuni ya Mt Albert wa Yerusalemu
Maandishi ya kiroho ya Watakatifu Wakarmeli kama vile:
Teresa wa Avila
Yohane wa Msalaba
Teresa wa Lisiuex (wa mtoto Yesu),
Pamoja na Watakatifu wengine Wakarmeli.
Na Katiba za Shirika.
Visivyoandikwa
Maisha ya Bikira Maria
Maisha ya Mtakatifu nabii Elia
Nabii Eliya
Kutamani kuwa kama Eliya kunaleta na kuchochea maisha ya ukimya, tafakari na kuishi katika uwepo wa Mungu. Maisha ya kumpenda Mungu zaidi ya kitu kingine chochote. Hali ya kutamani kukutana na Mungu kupitia Neno lake ambalo ni chakula cha kiroho. Roho hii kimsingi i katika hamu ya kuwa katika muungano na Mungu.
Maisha ya tafakari
Maisha ya kiroho ya wakarmeli yanajieleza kupitia tafakari na sala za ndani ya nafsi. Kuwa na hali ya ndani kabisa ya uwepo wa Mungu katika maisha ya mtu. Sala, ukimya wa ndani na upweke kwa ajili ya kuisikiliza sauti ya Mungu ndani ya nafsi zetu.
Kuwa na shauku ya wokovu wa wengine
Kuishi katika uwepo wa Mungu kunaleta bidii kwa ajili ya wokovu wa nafsi za watu. Huwezi kuongele maisha ya kiroho ya shirika bila kwanza kuongelea Kanuni ya shirika inayowataka wakarmeli waiishi wakiwe umakini katika Neno la Mungu. Kwa sababu maisha ya kiroho yanatokana na Kanuni yenyewe. Karama ni nini? Karama ni msukumo wa roho inayotaka kuishi fadhila fulani. Karama za shirika la karmeli imeelezwa katika maeneo matatu. Maisha ya sala, maisha ya kindugu na maisha ya huduma.