HISTORIA YA WITO WANGU
Kwa jina naitwa GODFREY CHRISTIAN ASSENGA. Nimezaliwa 23. 6. 1998 katika familia ya Bwana na Bi Christian Assenga. Ni mzaliwa wa Parokia ya Mt. Peter Claver Mengwe, Jimbo Katoliki la Moshi-Kilimanjaro, Jumuiya ya Mt. Maria wa Rozari.
FAMILIA
Familia ya Christian Assenga na Devota Peter ilibahatika kupata watoto saba [7], wa kiume sita [6] na wakike mmoja [1] mdogowetu wa kiume alifariki mwaka 2020. Mama yangu alifariki Tarehe 3 Aug 2003 na Baba alifariki Tarehe 18 Aug 2018. Namshukuru sana Mungu ambaye daima amekua mwema na mkarimu kwetu.
ELIMU
Nilihitimu darasa la saba mwaka 2012 katika shule ya msingi Kitukuni. Nikajiunga na shule ya sekondari St. John Vianney AMSP Maloa Moshi Kidato cha kwanza hadi cha nne, mwaka 2016-2019 na baadae shule ya Mapadre wa kazi ya Roho Mt. ALCP/OSS Bendel Memorial iliyopo Soweto Moshi kwa masomo ya kidato cha tano na sita mwaka 2020 - 2022..
WITO
Tangu utoto wangu nilikua na ndoto na tamaa kubwa ya kumtumikia Mungu kwa njia ya Upadre. Hamu hii ilidhihirika sana kupitia Misa Takatifu,maisha ya sala na ibada yangu kwa Ekaristi Takatifu na mama Maria. Pamoja na changamoto zote zilizoikaabili familia yetu Mungu alikua mwaminifu kwa wito wake kupitia mtumishi wake na alinipa moyo wa uvumilivu. Mwaka 2015 alinipa Fr. Mark Mlay ALCP/OSS na Sr. Jennifer Wandia AMSP kuwa wazazi wangu wa kiroho na hivyo ndoto yangu ya kuwa padre iliwaka kama mshumaa katika upepo mkali , asante Mungu kwa wazazi hawa wa dhamani.
[Fr. Mlay na Sr. Wandia ni wanzilishi wa shirika la masista wa Adore Missionary Sisters; AMSP.Na waasisi wa shule za St. John Vianney schools.
Mwaka 2016 walinipeleka katika shule yao nikasoma, nikakua katika malezi yao na baada ya masomo yangu nikawaelezea tena kwa ufasaha juu ya ndoto yangu kwa mara ya pili na hapo wakanipatia ruhusa ya kufanya chaguo ambalo pia litakua ni mapenzi ya Mungu. Kwa neema ya Mungu nilikutana na rafiki yangu, Frt. Frank Jonas Kageleka ALCP/OSS akanielezea karama za mashirika mbalimbali lakini nikavutiwa zaidi na shirika la WAKARMELI nikamweleza kwamba nitajiunga na Ndugu wa Karmeli na bila kusita aliniunganisha na Frt. John Madava ambaye pia ni Frateli mkarmeli alinipatia historia ya shirika na kunielekeza kwa mkurugenzi wa miito Fr. Victor Biramata O.Carm. Ni mkurugenzi huyu ambaye alinipatia maelekezo na kunielekeza vizuri sana katika kuifikia nia yangu hiyo nikajiunga na shirika 18 Aug 2022.
Yote kwaajili ya upendo wa Kristo kupitia moyo safi wa Maria.
Mama yetu Bikira Maria wa mlima Karimeli; Utuombee na utusaidie.