Mtawa mkarmeli, Mmistiko, mwandishi wa habari, mchapishaji na profesa
Alikufa akitetea haki za Kanisa
Familia yake.
Picha ya familia ya Brandsma. Huenda ilichukuliwa wakati wa upadrisho wa Tito mwaka 1905. Kutoka kushoto kwenda kulia: Fr. Tito, aliyebatizwa Anno, wa pili mdogo kabisa katika familia, Sr Maria, mmonaki wa faragha wa shirika la mafukara wa Clara, asingeweza kuwepo kwa sheria za kimonaki, picha yake ilichomekwa hapa baadaye. Jina la ubatizo lilikuwa Boukje. Mama yake Tito Tjitsje (POSTMA) Brandsma. Trees (hutamkwa "trace") de Boer, binti wa dada yake Tito aliyeolewa Gatske de Boer. Sr Willebroda, Masista wa Damu Takatifu. Jina la ubatizo lilikuwa Siebrigje. Jan de Boer, mwana wa dada yake Tito, Gatske. Gatske de Boer,mmoja tu kati ya kaka na dada zake Tito aliyeolewa. Padre Heinricus Brandsma, OFM, mdogo kabisa katika familia. Sr Barbara, Sista mfransiskani, alibatizwa Plone. Mikheil de Boer, shemeji yake Tito. Tito azaliwaTitus Brandsma alizaliwa tarehe 23.02.1881 Oegeklooster, Friesland mkoa wa kaskazini magharibi mwa kona ya Uholanzi. Jina lake halisi lilikuwa Anno Sjoerd Brandsma. Baba yake aliitwa Titus Brandsma–alikufa mwaka 1920 na mama yake aliitwa Tjitsje Postma –alikufa mwaka 1933. Walikuwa na watoto sita. Wasichana wanne na wavulana wawili. Familia yake ilikuwa ya kikatoliki kweli kweli. Dada zake watatu walikuwa wamonaki na kaka yake mwingine alikuwa Padre mfransiskani. Mtoto mmoja wa kike hakuingia utawa.
Shule
Alisoma seminari ndogo ya Wafransisko huko Megen, Uholanzi.
Anno alitamani kuwa padre tangu alipokuwa kijana mdogo. Akiwa na umri wa miaka 11, aliomba ruhusa kwa baba yake kuingia seminari ndogo ya wafransiskani huko Megen. Alikuwa kijana dhaifu na hakubahatika kuwa na nguvu kama watu wengine. Alikuwa tayari kufanya kazi ila hakuweza kutokana na afya yake. Tito naTjitsje, ingawa walikuwa na wasiwasi juu ya afya yake, walimpa ruhusa ya kwenda kujaribu seminari, na Anno aliondoka nyumbani kwao mwishoni mwa mwaka 1892.
Katika miaka yake sita akiwa Megen, Anno kijana wa Frisian alionekana mwenye akili ya kawaida na mtulivu. Alifanikiwa vizuri sana katika masomo yake. Utu wake ulimfanya apendwe na maprofesa na wanafunzi. Wanafunzi wenzake walimwita "de Punt," jina la utani maana "mfupi." Katika mwaka wake wa tatu, alipatwa na matatizo ya utumbo na kupoteza kwa kiasi kikubwa uzito. Ndugu (Friars) waliamuru kiwe kinaandaliwa chakula maalum kwa ajili yake, baada ya hapo afya yake iliimarika na kurudisha uzito wake. Yeye hivi karibuni zinalipwa afya yake na kurudi kwa nguvu upya kwa masomo yake na kuendelea vema na masomo yake. Hata hivyo, wakubwa wake, hawakuridhika kwamba alikuwa na nguvu ya kutosha kwa ajili misukosuko ya maisha ya Wafransiskani wa Uholanzi, walipendekeza kuwa atafute aina nyingine ya shirika linalomfaa. Anno alilikubali kwa neema na uthabiti.
Mwezi Septemba tarehe 17 1898, Anno alipiga hodi kwa Wakarmeli huko Boxmeer, Uholanzi, walimpokea kwa furaha kama mkandidati wao. Alibadili jina kama ilivyokuwa desturi ya wakati ule ikiwa ni ishara ya kuanza kipindi kipya cha maisha ya unovisi akiwa na umri wa miaka 17. Ndipo hapo alipochagua jina la Titus -Tito. Alichukua jina la baba yake.
Jumuiya ya Boxmeer ilikuwa na watawa 39, walitumia muda wao mwingi katika kusali, ukimya na upweke. Kufunga, kujinyima na kutafakari na utafiti wa maisha ya njia ya Karmeli. Anno-akiishi katika chumba cha kawaida, alilala juu ya godoro la majani, akiwa na vitabu juu ya dawati lake, kwenye hali ya utulivu alipiga magoti na kuingia katika sala ya utulivu, wakiimba usiku wa manane ofisio katika kanisa, kula vyakula rahisi, kujiumba kimya kimya na wenzake hapo alijua alikuwa amepata sehemu yake. Aliwaandikia nyumba hivi: "Nina furaha sana sasa".
Titus alianza kusoma na kutafsiri kazi za Mt. Teresa wa Avila ndipo walipogundua uwezo wake mkubwa wa kutafsiri. Tafsiri hizo ulikuwa mwanzo wa fasihi kwa muda mrefu na mafanikio ya kazi yake.
Tito pia alianzisha miradi kadhaa ya fasihi na wanafunzi wenzake katika miaka yake ya novisiati na baadae ya utafiti wa kimasomo. Aliwashawishi wenzake kujibidisha katika kuandika makala juu ya mada mbalimbali za kidini na alifanya kazi kama wakala wao na fasihi. Waliuuza makala zao kwenye magazeti ya Uholanzi na majarida. Aliendeleza kitengo cha uchapishaji cha Wakarmeli ambacho hatimaye kilitumiwa kwa shughuli za uchapishaji kwa ajili ya Wakatoliki wote wa uholanzi Uholanzi. Maandishi yake ya mwanzo yalionesha wazi kuvutiwa na mysticism kama kawaida ya Wakarmeli. Vile vile alionesha wajibu wa Mkristo wa kupenda haki za kijamii.
Nadhiri
Aliweka nadhiri zake za kwanza mwezi Oktoba 1899. Na kuruhusiwa kuendelea na masomo yake ya upadre.
Alipadrishwa Juni 17, 1905 akiwa na umri wa miaka 24 na kuruhusiwa kuendelea na masomo yake huko Roma.
Alikuwa Dokta wa falsafa huko Roma mwaka 1909 katika Chuo Kikuu cha Gregori (Pontifical Gregorian University October 25, 1909). Baada ya hapo alirejea tena Oss kwenda kufundisha falsafa huko Oss 1909-1923.
Mwaka 1901 akiwa bado mwanafunzi alichapisha kazi ya Mt. Teresa wa Avila iliyohusu maisha ya muungano na Mungu (Antolojia).
Mwaka 1916 aliunda timu ya wataalamu ya kutafsiri zaidi kazi za Mt. Teresa wa Avila.
Mwaka 1919 aliteuliwa kuwa mhariri wa gazeti la kila siku la kijamii. Alijihusisha na shughuli nyingi za kijamii. Pamoja na hayo ilifuata kwa kikamilifu ratiba ya maisha ya kikarmeli. Mwaka 1921 alikuwa amechoka sana na afya yake iliyumba sana. Lakini baadae alipata nguvu. Alitumia muda wake mwingi kuwasikiliza maskini na kuwasaidia wenye shida.
Aliitwa kufundisha falsafa na usufi (mysticism) na historia ya umistiko katika Chuo kikuu cha Nijmegen mwaka 1923. Baadaye alichaguliwa kuwa mkuu wa monasteri ya Nijmegen.
Mwaka 1932 alichaguliwa kwa mwaka mmoja kuwa rector magnificus, rais wa Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Nijmegen. Aliwaunganisha wakufunzi na kuonesha uwezo mkubwa wa kuongoza.
Mwaka 1935 aliteuliwa na askofu mkuu wa Utrecht kuwa mshauri wa kiroho wa umoja wa waandishi wa habari wa kikatoliki wa Uholanzi. Ni katika mwaka huo alitembelea Amerika kwa ziara ya uandishi wa habari.
Tarehe 10 mwezi wa 5 Mwaka 1940 jeshi la Adolf Hitler lilivuka na kuingia Uholanzi. Shule za kikatoliki ziliamuliwa kuwafukuza wayahudi. Mishahara yao ikapunguzwa kwa asilimia 40. Titus alipingana na hali hiyo. Titus alisema hapana kwa wanazi.
Askofu Mkuu De Jong alimkabithi Titus jukumu la kuwaambia waandishi wa kikatoliki kuwa jibu la Kanisa ni hapana kwa wanazi ambao walitaka kutumia vyombo vya habari vya kikatoliki kueneza propaganda zao. Lakini alimtahadharisha kuwa kazi hiyo ilikuwa hatari. Titus alikubali na kuifanya kazi hiyo.
Kukamatwa kwake –aliitwa Mtawa hatari
Alikataa kuchapisha propaganda za kinazi kwenye magazeti ya Kikatoliki
Titua alikuwa ameisha tembelea wahariri 14 kabla ya kukamatwa na Gestapo siku ya jumatatu ya tarehe 19 Januari mwaka 1942 saa 12 za jioni. Alikamatwa kwenye monasteri ya Boxmeer. Alipiga magoti n akupokea Baraka toka kwa mkubwa wake. Aliondoka akiwa amevaa mavazi meusi ya ukasisi. Polisi walimchukua chini ya ulinzi na kumpeleka kwenye gereza la Scheveningen. Akafungiwa kwenye chumba namba 577. Alimwambia afisa aliyemkamata “fikiria mimi kwenda jela na umri wa miaka 60”. Yule afisa akamjibu “usingekubali kazi uliyopewa na maaskofu”. Inafahamika wazi kuwa alipinga sera za chama cha national -socialist ideology na wanazi.
Kapteni Hardegen alimuuliza Titus, “kwa nini ulikaidi amri za utawala”, Titus akamjibu “kama Mkatoliki nisingefanya vinginevyo”.
Tarehe 21 Januari mwaka 1942 akaambiwa kuwa atakaa jela kwa muda. Aliambiwa kuwa kwa kuwa yeye ni mmonaki maisha ya jela hayatakuwa magumu kwake.
Akiwa jela kwa wiki 7 huko Scheveningen aliandika mashairi na kuandika tafakari za njia ya msalaba. Alikuwa akipiga magoti kama ilivyokuwa kawaida yake ni kusali. Anashuhudia kuwa huko jela maisha yaliendelea kama kawaida, aliandika, alisali na alikuwa mtulivu.
Tarehe 12 mwezi machi akiwa na wenzake 100 alihamishiwa kwenye gereza la Amersfoort. Walipofika pale waliambiwa wasimame kwenye mvua ya baridi ya mgando kwa masaa kadhaa. Baada ya hapo wakapelekwa kwenye chumba za kuvalia nguo. Walivuliwa nguo na kuamriwa kurudi tena kwenye mvua. Walikuwa wakitetemeka. Baada ya hapo wakapewa nguo za wafungwa.
Waombeeni watesi wenu
Mapadre walipigwa marufuku kutoa huduma za kiroho gerezani. Lakini Titus alikaidi amri hiyo. Ijumaa Kuu aliwakusanya watu na kuongoza tafakari ya mateso ya Yesu Kristo. Alikuwa akisikiliza maungamo na kuwatembelea wagonjwa waliokuwa wakifa hospitalini. Aliwasihi wafungwa walioteswa wasali na kuwasamehe watesi wao.
Mwishoni mwa mwezi wa 4 Gestapo aliamuru Titus arudishwe Scheveningen kutoka Amersfoort kwa mahojiano zaidi. Alisisitiza kuwa Titus alikaidi sheria za utawala.
Baadaye alitaarifiwa kuwa itahamishiwa Dachau. Aliomba afungwe kwenye jela ya kikarmeli huko Ujerumani lakini alikataliwa. Wakati huo alikuwa Kleve Ujerumani akiwa njiani kupelekwa Dachau.
Alipofika kwenye kambi ya mateso ya Dachau aliteswa sana na kupigwa. Kambi hii ilikuwa na kikanisa cha kuadhimishia ibada. Lakini wafungwa hawakuruhusiwa kuhudhuria.
Gerezani siku ilianza saa 10 asubuhi na kuisha saa 1 jioni kwa kazi ngumu na adhabu. Kipindi hicho tayari Titus alikuwa ameadhirika na sumu iliyokuwa ikiutafuna mwili wake.
Hapo awali alikataa kwenda hospitali baada ya hali yake kuwa mbaya. Lakini baadaye alikubali kwenda hospitali. Kama ilivyokuwa kwa wafungwa wengine kufanyiwa majaribio ya kisayansi, hata yeye alifanyiwa majaribio.
Pamoja na mateso aliwahi kusema hivi akiwa katika kambi ya mateso
Mimi namwona Mungu katika kazi ya mikono yake na alama ya upendo wake katika mambo yote yaonekanayo. Mimi nimekamatwa na furaha kuu ambayo ni zaidi ya furaha nyingine zote.
Kifo chake
Mchana wa jumapili tarehe 26 Julai mwaka 1942, daktari aliyekuwa akimsimamia aliamuru achomwe sindano ya dawa za kufisha (sumu). Ndani ya dakika 10, Titus aliyeishi kwa furaha akiwafariji wengine alikuwa amekufa. Alifia Dachau Bavaria, kambi ya mateso Ujerumani.Baada ya kufariki dunia mwili wake ulichomwa moto.
Alitangazwa mwenye heri tarehe 3.11.1985 na Papa Yohane Paulo II.