Historia fupi ya Kitaaluma
Kwa jina naitwa Athanas Mhina Ngassa, nilizaliwa tarehe 04/07/1992 katika familia ya Baba Simon Ngassa na Mama Maria Nyanzala. Nimekulia katika kijiji cha Lugunga kilichopo wilaya ya Mbogwe, mkoa wa Geita. Niliianza safari ya masomo ya awali Mwaka 2000, na mwaka 2001 nikaandikishwa rasmi kama mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Lugunga. Mwaka 2007 nilimaliza masomo ya shule ya msingi na nikafaulu kuendelea na masomo ya sekondari. Mwaka uliofuata, yaani 2008 nilichaguliwa kujiunga na Sekondari ya Lugunga, hapo nikaanza safari ya elimu ya kidato cha kwanza hadi cha nne na nikahitimu mwaka 2011. Baadae nilichaguliwa kujiunga na Shule ya Sekondari Kigoma kwa masomo ya kidato cha tano na cha sita. Hivyo, Mwaka 2012 nilianza masomo hayo nikichukua mchepuko wa HGL, mwaka 2014 nikafanikiwa kumaliza masomo hayo. Mwaka huohuo, nilijiunga na Shirika la Mapadre wa Mwenye Heri Sana Bikira Maria wa Mlima Karmeli Bunju, Dar es Salaam. Nilianza malezi na mwaka 2015, nikaanza masomo ya Shahada ya Falsafa katika Chuo kikuu kishiriki cha Mtakatifu Augustino- Tawi la Jordan Morogoro. Mwaka 2018 nikamaliza stashahada ya kwanza ya Falsafa. Niliomba maombi ya kuendelea na Unovisi na nikapokelewa na hivyo nikatumwa Nchini Zimbabwe kwa mwaka mmoja tangu 2018-2019, na mwaka 2019 mwezi Novemba nikajiunga na chuo Cha Jordan kwa stashahada ya masomo ya Taamuli Mungu ( Theolojia), hivi sasa nimemaliza mwaka wa kwanza wa masomo hayo yatakayoendelea mpaka mwaka 2023. Ninamshukuru Mungu kwa Baraka zake nyingi kwangu. Nawashukuru wazazi na ndugu wote na wote wanaendelea kunisaidia kufikia malengo Kristo aliyoyaweka kwangu. Kwa Upekee nalishukuru Shirika langu kwa kuniamini na kuniruhusu niendelee na masomo ya Taamuli Mungu. Kwangu safari ya kitaaluma naiona ni njia ya kutimiza lengo ambalo Mungu ameliweka ndani mwangu.