Nyazura Zimbabwe
Leo terehe 05/07/2024 wanafunzi watatu wa shirika la Karmeli,wameondoka kwenda Zimbabwe kwa hatua muhimu sana ya unovisi. Walisindikizwa na wenzao,
Ndg; Charles Masibuka, Joseph Peter, Magnus Tibasanirwa, Simon Karoli, Padre Dominic Somola na Padre Victor Biramata.
Mama Karmeli nchini Tanzania anafuraha kubwa sana leo hasa anaporuhusu na kuwatuma rasmi viijana wake watatu, Ndg; John Kheri Madava, Faustine Innocent Nh'umbili, na Ansbert Protas Mulaly kwenda nchini Zimbabwe kwa ajili ya hatua nyingine ya malezi (unovisi) yatakayodumu kwa muda wa mwaka mmoja, Julai 2024/ Julai 2025. Vijana hao walihitimu rasmi elimu yao ya masomo ya Falsafa katika chuo kikuu kishiriki cha Mwenyeheri Jordan pale Morogoro.
Leo tarehe 05.07.2024 wamesindikizwa mpaka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na familia ya Wakarmeli akiwemo mwakilishi wa Mkuu wa Komisarieti ya la Bruna Napoli Padre Dominic Somola, Padre Victor Biramata, Ndg; Charles Masibuka, Joseph Peter, Magnus Tibasanirwa na Simon Karoli.
Tunawaombea kila jema katika hatua hiyo muhimu sana katika malezi yao ya kitawa na safari ya upadre wanaoutamani. Mama yetu wa Mlima Karmeli azidi kuwafunika kwa scapulari yake na kuwahifadhi katika nchi ya ugenini. Mama na ua zuri la Karmeli Utuombee. Amina...