Mungu aliumba
Mtu: mwanaume na mwanamke (Mwa 1:26-27). Majina yao: Adamu (Mwa 2:20) na Eva (Mwa 3:20). Mwanaume na mwanamke wote wawili wanaitwa Adamu (Mwa 5:2).
Waliwekwa –Edeni (Mwa 2:8). Uasi wao (Mwa 3:1-7). Kufukuzwa kwao (Mwa 3:23-24).
Watoto wao wa kwanza: Kaini (Mwa 4:1), Habili (Mwa 4,2). Kaini alimwua Habili nduguye (Mwa 4:8).
Nuhu: mtoto wa Lameki: (Mwa 5:29-30). Alijenga safina kubwa kuikoa familia yake na wanyama (Mwa 6:14-22; 7:7-8). Agano na Mungu (Mwa 9:8-11). Upinde wa mvua ishara ya agano (Mwa 9:12-17). Watoto wa Nuhu: Shemu, Hamu,Yafethi (Mwa 9:18).
Abramu: mtoto wa Tera (Mwa 11:26). Abramu akamwoa Sarai (Mwa 11:29). Abramu anapewa jina la Ibrahimu (Mwa 17:5). Sarai anapewa jina la Sara (Mwa 17:15-16). Abramu alipewa Hajiri mjakazi wa Sarai kama mke, akamzalia mtoto akamwita Ishmaeli (Mwa 16:1-16). Ibrahimu akazaa na Sara mtoto wa ahadi, jina lake Isaka (Mwa 17:19.21; 21:1-3). Ibrahimu alimwoa mwanamke mwingine aliyeitwa Ketura (Mwa 25:1). Ishmaeli alifukuzwa (Mwa 21:9-21). Ibrahimu akataka kumtoa mwanawe Isaka sadaka (Mwa 22:1-19).
Isaka: akamwoa Rebeka (Mwa 24:67). Isaka akazaa na Rebeka watoto wawili mapacha: Esau na Yakobo (Mwa 25:24-26). Esau akauza haki ya mzaliwa wa kwanza kwa mdogo wake Yakobo (Mwa 25:27-34). Yakobo akachukua mbaraka wa Esau (Mwa 27:1-28:9).
Yakobo: (Israeli (Mwa 32:28)) alipata watoto kumi na wawili ambao pamoja na familia zao ndiyo mababa wa makabila kumi na mawili ya Taifa la Israeli (Mwa 29:31-30:22). Majina ya watoto hao ni haya yafuatayo: 1. Reubeni (Mwa 29:32), 2. Simeoni (Mwa 29:33), 3. Lawi (Mwa 29:34), 4. Yuda (Mwa 29:35), 5. Dani (Mwa 30:6), 6. Naftali (Mwa 30:8), 7. Gadi (Mwa 30:11), 8. Asheri (Mwa 30:13), 9. Isakari, 10. Zabuloni, 11. Benyamini, 12. Yosefu. Watoto hawa kumi na wawili walizaana na kuongezeka sana (Kut 1,7). Mungu akawateua kuwa taifa teule (Kumb 10:15).