Wakarmeli wanatafuta kuishi maisha ya tafakari au kwa lugha nyingine maisha ya taamuli. Watu wanaomtafuta Mungu. Wanaotamani kubadilishwa naye. Maisha ya kiroho ya wakarmeli yanatokana na karama za shirika: Maisha ya kindugu, Maisha ya huduma, na Maisha ya taamuli/tafakari.