Â
Nadhiri za daima Napoli Italia
Shirika la wakarmeli linafanya utume wake katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam, katika parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli bunju. Makao makuu ya shirika yako Roma Italia. Mpaka sasa lina mapadre sita watanzania. Konventi ya shirika iko bunju "A".
Nembo ya shirika la wakarmeli O.Carm upande wa kushoto na la wakarmeli O.C.D upande wa kulia.
Konventi ya wakarmeli wa bunju
Wanafunzi wakarmeli wanaofanya uzoefu wa maisha ya wakarmeli, maisha ya kitawa kwa lengo la kujiunga na shirika la wakarmeli. Wako malezi bunju wakijiandaa kuanza falsafa mwakani.
Skapulari. Skapulari ni nyenzo inayofaa kwa ajili ya kumheshimu Bikira Maria. Ni kiashiria cha wokovu. Ni ishara ya ulinzi na upendo wa Bikira Maria kwa wakarmeli.
VIJANA WA PAROKIA
Vijana wa parokia wakijiandaa kwenda hija bagamoyo. Vijana wanahitaji kulelewa vizuri kwa lengo la kukuza imani yao. Hawa vijana ndio WAWATA wa kesho na UWAKA pia.
Upadrisho Mbezi Luis
Siku ya upadrisho wa padre Paul Malewa, padre Victor Biramata, padre Paschal Shirima, na mapadre wengine wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam na mmoja wa shirika Salestiani.
Ikoni ya Bikira Maria wa Karmeli
Ikoni ya Bikira Maria wa Karmeli. Huu ndio mchoro wa kale zaidi katika historia ya Shirika la wakarmeli. Hujulikana kama "la Bruna". Ikoni hii inahifadhiwa katika basilika la Carmine Maggiore Napoli, Italia. Kopi ya hii Ikoni iko kwenye kikanisa cha wakarmeli bunju.Maelezo ya Ikoni
WAKARMELI WATANZANIA
Kwaya ya Mtakatifu Yosefu Bunju
Kwaya ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli Bunju
KARAMA ZA SHIRIKA
Kuishi maisha ya utii kwa Yesu Kristo na kumtumikia Yeye kwa uaminifu, kwa moyo safi na kwa dhamiri njema: Maneno haya ya uvuvio ya Mt. Paulo Mtume, ndiyo msingi wa mambo yote ya karama yetu. Yamekuwa msingi ambao juu yake Albert alijenga njia ya maisha yetu. Wakarmeli tuna karama tatu.
NABII ELIYA
Nabii Eliya anatajwa katika kitabu cha kwanza na cha pili cha Wafalme (1Fal 17:1). Aliishi kwenye karne ya 9 K.K wakati wa utawala wa mfalme Ahabu. Aliteswa na mfalme Ahabu (1Fal 17:2-7). Alilishwa kwa miujiza na kunguru (1Fal 17:2-7). Alitetea kuabudu Mungu wa kweli. Alikaa siku arobaini bila kula (1Fal 19:8). Bikira Maria na Skapulari
LITURUJIA
Hili ndilo kundi la wakarmeli wa kwanza kufika kuanzisha misheni Tanzania 2009.