Naitwa Saimon Karoli Sigisbert nimezaliwa tarehe 15/09/2001 katika Jimbo la Morogoro, Parokia ya Mhonda kabila langu ni (Iraq) Mbulu. Ni mtoto wa tatu (3) kati ya watoto (7) saba, kwa Mgawanyiko wa jinsia ya watoto katika familia, wakike (4) na wakiume (3)
Baba yangu Koroli Sigisbert Basso ni mzaliwa wa Arusha, kabila lake ni Iraq kutoka Jimbo kuu la Arusha, Parokia ya Rhotia Mama yangu Rebeka Jella ni mzaliwa wa Arusha kabila lake ni Mbulu. Kabla ya ndoa mama alikuwa dhehebu la KKKT lakini kwa sasa wazazi wote ni wakristo wa kanisa katoliki na wanashiriki Masakramenti.
Nilipata Sakramenti ya Ekaristi Takatifu 29/12/2012 katika Parokia ya Mhonda, pia Sakramenti ya kipaimara 01/10/2017 chini ya Askofu Thelesphodi Mkude, alimtuma mwakilishi wake Fr. Kasian Mkwadu ambaye kwa sasa ni marehemu.
ELIMU
Elimu yangu nilianza kupata katika shule ya msingi, Dihinda mwaka 2008 hadi 2015 kwa ngazi ya elimu ya msingi na kupata ufaulu mzuri wa kuendelea na elimu ya Sekondari.
Mnamo mwaka 2016 nilijiunga na elimu Sekondari katika shule ya sekondari Kanga Hill hadi mwaka 2019 na kuhitimu kidato cha nne na kupata ufaulu wa kuendelea na kidato cha tano (Advance level).
Mnamo mwaka 2020 nilijiunga na elimu ya A-level katika shule ya Alfagems Sekondary hadi mwaka 2022 na kupata ufaulu wa kawaida.
Mnamo mwaka 2022 nilianza kufanya mchakato wa kutafuta shule ya kurudia mtihani wa kidato cha sita na kupata ufaulu wa division II ya point 12 iliyoniwezesha kuendelea na ngazi nyingine.
Mnamo tarehe 06/07/2023 nilimtafuta Fr. Deogratius kwa kumshirikisha wito wangu na matokeo yangu ya kidato cha sita. Yalianza mawasiliano na Mkurugenzi wa miito Fr. Victor kwa kuomba nafasi ya kujiunga katika shirika la Carmelite Order (O. Carm), ilipofika tarehe 31/08/2023 nilifanikiwa kuwasili pamoja na Fr. Victor katika nyumba ya Mapadri iliyopo Bunju.
STORI FUPI KUHUSU WITO
“Mimi hapa Bwana nitume, Isa 6:8” nikiwa na umri wa miaka 10 niliokota picha ya Yesu yenye msalaba na muonekano mzuri nilipo ipelekea nyumbani wazazi na ndugu zangu waliniambia nimwombe Mungu anionyeshe mwanga. Nilimwomba Mungu lakini sikutambua chochote.
Nilipofika kidato cha tatu nilipenda sana kuijua Biblia hasa historia kuhusu kanisa katoliki na kupenda kuanza tafakari juu ya neno la Mungu. Pia niliendelea kufanya tafakari nikiwa TYCS.
Nikiwa kidato cha tatu alikuja Paroko shule na kutupa habari kuhusu kumtumikia Mungu hasa kwa daraja la upadri ni kipindi ambacho kiliniwazisha na kuwaza juu ya habari hii. Pia nilimshirikisha padri baada ya kumaliza kidato cha nne nilianza kupata msukumo mzito juu ya kumtumikia Mungu. Nilipata rafiki ambaye tulikuwa tunashauriana juu ya safari hii pia baada ya kumaliza kidato cha sita matokeo yangu haya kuwa mazuri. Ilinibidi nirudie mtihani na baada ya matokeo kuwa mazuri nilimshirikisha Fr. Deugratius Baharia na kunishauri na kunielekeza juu ya shirika la wakarmeli.
Mnamo tarehe 07/08/2023 nilielekea pamoja na Father. Katika nyumba ya wakarmeli iliyopo Morogoro maeneo ya Kola nilikutana na Fr. Victor Biramata na kutupokea vizuri tulisalimiana vizuri na Fr. Victor pia niliwakuta Mafratelli wawili pia nilipiga nao stori na kunikaribisha sana katika shirika la wakarmeli.
Nilifanya mahojiano na Fr. Victor Biramata na baadae tulipanga siku nyingine ya kukutana tarehe 25/08/2023 tulikutana na kunihoji Zaidi kuhusu wito wangu na baadaye kunipangia tarehe ya kuelekea nyumba ya malezi iliyopo Dar es salaam. Ilipofika tarehe 31/08/2023 tulipanga safari pamoja na Fr. Victor Biramata na kuelekea Dar es salaam safari ilikuwa nzuri sana pia na matukio ya kushangaza barabarani. Tuliwasili Dar es salaam mnamo saa 5:00 jioni nilipokelewa na Frt. Felix na kuelekezwa chumba cha kukaa. Usiku wangu wa kwanza katika chumba changu nilipata usingizi mzito na ilipofika asubuhi nilianza kuendelea na kupewa maelekezo mbalimbali kutoka kwa kaka niliyowakuta.
Namshukuru Mungu sana kuwepo katika shirika la Karmeli pia nazidi kufurahia maisha yangu ya jumuiya.
BIKIRA MARIA MAMA YETU WA MLIMA KARMELI, UNIOMBEE.