SOMO LA NAFASI YA BIKIRA MARIA KATIKA UKOMBOZI
KUHUSIANA NA SKPAULARI
1. UTANGULIZI WA MADA ZETU.
Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza (Rum 8:28-30). –Hii hutokea ukikubali utawala wake na unapokubali utumike.
2. Mwanadamu anapokea kutoka kwa Mungu na anatoa bure.
Na katika kuenenda kwenu, hubirini, mkisema, Ufalme wa mbinguni umekaribia.
Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure (Mt 10:7-8).
3. Bikira Maria anatoa Skapulari –Nguvu yake iko katika imani na neema.
Njia zinazotumika ni mbalimbali.
· Huduma za Kanisa.
· Maisha
· Mazingira
· na vitu vinavyomfaa mwanadamu.
Visakramenti daima vinaambana na sala na ishara -kwa mfano kuwekewa mikono, ishara ya msalaba na mnyunyizo wa maji.
Visakramenti hutokana na ukuhani wa ubatizo -kila mtu ameitwa kuwa "baraka" na kubariki. Utasikia watu wanasema Mungu akubariki. Wazazi huwabariki watoto.
5. Kuwa baraka na kubariki
Visakramenti havitoi neema ya Roho Mtakatifu. Ila vinatuandaa kuipokea neema na kisha kushirikiana nayo.
Hakuna kitu chochote ambacho kikitumika vizuri kinashindwa kumwandaa mtu kupata neema.
6. Visakrameti katika Maandiko Matakatifu
Musa na fimbo ya Aroni –Fimbo yenye uwezo wa miujiza.
Fimbo ya Musa inaweza kuchukuliwa kama kisakramenti.
Musa alitumia fimbo aliyooneshwa na Mungu kufanya maajabu na kusaidia Taifa Teule la Israeli kutoka utumwani Misri (Kut 4:17). Kuvuka bahari ya shamu (Kut 14:15-16).
Fimbo ya Aroni inahifadhiwa katika sanduku la agano (Ebr 9:4). Kwa habari zaidi soma Kitabu cha Kutoka sura ya 17.
Hivyo visakramenti vina nguvu fulani ya kumiujiza (1Fal 2:8).
7. Maana ya baraka
Kubariki ni tendo la kimungu lenye kutoa uzima na Baba ndiye chemchemi. Ni kukutana kwa Mungu na mwanadamu. Mtu anapokea paji la Mungu. Moyo wa mwanadamu waweza kumbariki Yeye nayeubariki.
Ule uzima unakifanya kitu, au mtu awe na nguvu fulani ya kimungu ya kupingana na mwovu.
8. Aina mbalimbali za Visakramenti
Baraka zote -Kanisa linatoa baraka kwa kuliitia jina la Yesu na kwa kufanya ishara ya msalaba. Baraka zote na maombi kwa jina la Yesu Kristo. Kubariki watu, vyakula, vitu na mahali.
Baraka za kudumu za vitu au mahali kwa ajili ya matumizi ya Liturujia - Kutabaruku kanisa -kubariki Makanisa au altare, kubariki mafuta na vyombo vya liturujia na mavazi, na kengele --- au kuwatoa watu kwa Mungu- mfano abate au abatesa wa monasteri, ibada ya nadhiri za watawa, kuweka wakfu mabikira na wajane, baraka kwa wahudumu fulani, wasomaji, makatekista. . Lile tendo la kuvibariki ni kisakramenti.
Uwingaji -(kupunga nguvu za mwovu) -Kanisa linapotumia mamlaka yake kwa kuliita Jina la Yesu Kristo ili mtu akingwe dhidi ya nguvu ya yule mwovu na kumtoa kutoka utawala wake. Uwingaji wa kawaida (mdogo) hufanyika kabla ya ubatizo. Uwingaji mkubwa hufanywa kwa mamlaka ya Kanisa.