J.M.J.E
«... Yesu akamwambia, Mama, tuna nini mimi nawe? Saa yangu haijawadia.” Mamaye akawaambia watumishi, “ Lolote atakalowaambia fanyeni...» [ Yoh. 2, 4-5 ].
«... Unafanya nini hapa Eliya?” Akasema, “ Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana, Mungu wa majeshi; kwa kuwa wana wa Israeli wameyaacha maagano yako, na kuzivunja madhabahu zako, na kuwaua manabii wako kwa upanga; nami nimesalia, mimi peke yangu; nao wanataka wanitafuta roho yangu waiondoe...» [ 1 Fal 19, 9-10 ].
Kumbukumbu ya Upadrisho
Wa
Dominic John Maria Somola O. Carm
Shirika la Bikira Maria wa Mlima Karmeli
Ushemasi {Diaconato} 6.5.2011. Parokia ya Mwenyeheri Isidori Bakanja- Boko na Mha. Askofu Salutaris Libena – Aliyekuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar Es Salaam.
Upadrisho{Presbitero} 24.8.2012 Kigango cha Mt. Yosefu Bunju - Parokia ya Mwenyeheri Isidori Bakanja na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar Es Salaam.
Misa za Shukrani
Sifa, Shukrani na Utukufu wa Mungu ziwaendee Wazazi, kaka na dada zangu, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki waliohai na waliotangulia, walioniombea na kunisaidia kuijongea Altare ya Bwana.
Wapumzike kwa amani { Eterno riposo}; marehemu Babu Mzee Somola, Kaka yangu Renatus na wote waliotamani kuiona siku ya Upadrisho wangu.
Bikira Maria wa Mlima Karmeli Utuombee.