Walipofika walipokelewa vizuri na mapadri Wakarmeli na wakapata nafasi ya kuwasalimia waamini wa bunju. Siku ya jumatatu ya tarehe 12.09.2016 walikutana na timu inayoshughulikia ujenzi na contractor Massimo. Katika mkutano huo walifanya marekebisho muhimu na wakakutana tena tarehe 17.09.2016 kwa ajili ya kuyakamilisha. Baada ya kukamilisha marekebisho hayo, wameondoka leo tarehe 21.09.2016 kurejea nchini kwao Italia. Lakini wameahidi kurudi tena kwa ajili ya kuangalia kazi inavyoendelea. Uwepo wao umezidisha matumaini mapya ya kuanza ujenzi wa kanisa. Wanafanya kazi hiyo kwa furaha kwa sababu, daima wamesema kuwa ni sehemu ya shukrani yao kwa Mungu kwa yote aliyowatendea na ni sehemu ya umisionari wao kwa kuwa wao ni Wakristo. Wamewaomba waamini wa bunju kujitoa na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuhakikisha kanisa linajengwa. Msanifu Flavia alinukuu msemo wa Mt. Calcutta kuwa inatosha tone la maji kutengeneza bahari. Wakati huo Prof. Renato amesema kuwa yeye atafurahi kushiriki na waamini wa bunju kwenye misa ya kwanza itakayofanyika katika kanisa jipya. Iwe yu hai hapa duniani au awe amekufa. Walionesha furaha yao kuona kuwa sasa ujenzi utaanza wakati wowote kuanzia sasa. Waamini wa bunju walifurahi na kuwatakia safari njema.