Mwaka 2014 Julai vijana wanne walifika Bunju kuanza uzoefu wa maisha, ya Karmeli. Baada ya mwaka mmoja wa uzoefu, walipenda maisha ya Wakarmeli na kuteuliwa na Shirika kuendelea na malezi. Tarehe 2 Novemba, 2015 walifika Morogoro kuanza falsafa kwenye Chuo cha Jordan (Jordan University College). Majina yao ni Dicksoni Sambala, Athanas Ngasa, Pascal m. Dominic na Deogratias Peter. Kulingana na changamoto za malezi na wito kijana mmoja aliondoka na kurejea nyumbani mwaka 2016. Kwa sasa kuna wanafunzi tatu (3) (postulants) ambao wamemaliza mwaka wa kwanza wa falsafa. Baada ya masomo ya falsafa, kwa wanao chaguliwa kuendelea, hutumwa nchini Zimbabwe kwa ajili ya noviziato. Wanafunzi waliobaki baada ya kuondoka kwa mwanafunzi mmoja. Mwaka huu wa 2016 wanaingia mwaka wa pili wa falsafa. Mwaka huu wa 2016 tunatarajia kupokea vijana wengine. Vijana hawa wanatoka kwenye shule za sekondari na vyuo mbalimbali.
Dickson Sambala
Alizaliwa 18.9.1981. Alisoma kidato cha tano na sita kwa mfumo wa QT –Mbezi Beach High School na kuhitimu mwaka 2014. Aliingia Karmeli kuanza malezi (uzoefu -experience) tarehe 22.7.2014. Alianza masomo ya falsafa mwaka 2015 katika Chuo Kikuu kishiriki cha Jordan Morogoro.
Athanas Ngasa
Alizaliwa tarehe 4.7.1992. Alihitimu kidato cha sita huko Kigoma Sch mwaka 2014. Aliingia Karmeli kuanza malezi (uzoefu-experience) tarehe 17.7.2014. Alianza masomo ya falsafa mwaka 2015 katika Chuo Kikuu kishiriki cha Jordan Morogoro.
Pascal Dominic
Alizaliwa tarehe 12.4.1993. Alihitimu masomo ya kidato cha sita mwaka 2014 huko High School –Mpwapwa 2014. Aliingia Karmeli tarehe 21.7.2014 kuanza malezi (uzoefu-experience). Alianza masomo ya falsafa mwaka 2015 katika Chuo Kikuu kishiriki cha Jordan Morogoro.