Somo la Ikoni
Ikoni ya Maria “La Bruna” ni picha kongwe zaidi ya Maria ailiyokubaliwa na Wakarmeli. Muundo wa unatoa maelezo ya kuvutia yanayo saidia kuelewa tunu za utu wa Maria na ina tunu ambazo zinatakiwa ziwe msukumu wa maisha ya kimaria na kuwa na ibada kwa Maria. Katika picha hii tunakutana na vipengele vifuatavyo vya ishara na maelezo ambavyo tunavitolea ufafanuzi wa maana zake kulingana na kanuni za uchoraji wa kipindi hicho: 1. Mduara wa dhahabu (Dhahabu = rangi ya jua) na nyuma yake kuna dhahabu ya Ikoni inayoonesha utakatifu wa Mama na Mtoto, wanaotegemezwa na uwepo wa Mungu.
2. Rangi ya maji ya kijani (Ishara ya uzazi) ya vazi la Maria inatangaza umama wake wa kimungu.
3. Rangi nyekundu (ishara ya upendo) ya kanzu chini ya vazi ambalo sehemu moja inamfunika Mtoto inaonesha nguvu na wepesi wa upendo wa Mama kwa Mtoto wake Yesu.
4. Nyota na mkia unaoning’inia katika vazi la Maria ni ishara ya Ubikira wa daima, kabla, wakati na baada ya kuzaa.
5. Rangi (ngozi ya kondoo) ya vazi la Mtoto inatuonesha: tazama hapa Mwanakondoo wa Mungu.
6. Uso wa Mtoto hauoneshi mwonekano wa kitoto, unajaribu kuonesha Umungu wa Neno aliyefanyika mwili.
7. Mkono wa kushoto wa Maria, uliombeba salama Mtoto, ni alama ya huruma. Mkono wa kulia ni jibu kwa ombi letu: “Utuoneshe Yesu mzao mbarikiwa”, unatuonesha: “Tazama Njia, Ukweli na Maisha”.
8. Nyuso za Mama na Mtoto zimegusana kieleleza cha uhusiano mororo.
9. Macho ya Maria na ya Yesu yanatutazama, mbali ya Ikoni, na yanaeleza hivi Kazi ya ukombozi ya Yesu na ushirikiano wa Maria katika Ukombozi huo.
Utungaji huu wa uchoraji wa ikoni wenye asili ya kigiriki au wa huruma, unaongea na mkarmeli na kwa mwenye ibada kwa Maria juu ya uhalisia wa Bikira Maria Mama wa Mungu katika fumbo la Kristo na la Kanisa, na ni mwito wa uhusiano wa karibu sana, wa kifamilia na wa kumwiga Yeye na Mwanae Mungu, Bwana wetu....
“Inawezekana kufahamu vilio vya roho zisizo na idadi ambazo zimetoa sauti mbele ya hii Ikoni kwa karne nyingi. Macho ya Mama yanafuatilia safari ya kila mtu, hakuna kinachozuia asione, hakuna kinachozuia kukimbilia moyo wake wa kimama....”
TENDO LA KUJIKABIDHI
Ee Bikira wa Karmeli,
Madonna Bruna.
Mama wa Karmine, kama kwa karne wanavyopenda
kukuomba taifa la Tanzania,
ujaze uwepo wako safari yetu ya maisha.
Uzuri wako, kioo cha Uzuri wa kimungu,
Utusaidie kumpenda Mungu na ndugu zetu,
Kwa moyo safi na kwa kujitolea kikamilifu.
Hekima yako,
Zawadi ya Roho Mtakatifu,
Ituelimishe kusilikiliza kwa sala Neno kuishi kadiri ya Kusudi lake.
Ukaribu wako
Ishara ya ahadi ya Mungu
Utufundishe mshikamano na upendo kwa maskini.
Kwa mfano wako, ututegemeze ewe Maria, Mama yetu na dada yetu. Amina.