Mnara wa Kanisa la Bikira Maria wa Mlima Karmeli Napoli
Kanisa la Karmine Napoli Italia
Misheni ya Shirika la Wakarmeli wa Tanzania-O.Carm iko chini ya Komisarieti ya “La Vergine Bruna” yenye makao makuu yake Napoli Italia. Komisarieti hii ilitangazwa hivi karibuni kwa jina hili. Lakini hata hivyo imerithi utamaduni ambao ni wa tangu mwaka 1524. Wakati ambapo konventi ya Napoli “Carmine Maggiore”, hata kama ilibaki kuwa jumuiya ya provinsi ya Neapoli, ilipoondolewa kutoka kwenye mamlaka ya provinsi hiyo mara moja na kuwekwa chini ya mamlaka ya Mkuu wa Shirika. Baada ya muda, nyumba hiyo ilipewa maeneo mbalimbali ya makazi (Kwa 1617 ilimiliki kumi na tano). Mwaka 1631 mageuzi (mabadiliko) ya Santa Maria de Vita yalizaliwa kutoka kwenye hii konventi na hatimaye iliongezewa ndugu (mafrateli) kutoka konventi nyingine hivyo mageuzi yakateuliwa kuwa provinsi mwaka 1660. Katika mwaka wa 1725 ikateuliwa “Provinsi ya Napoli” na iliundwa na konventi kumi na moja za “Carmine Maggiore”, konventi tano kutoka Provinsi ya Neapoli na konventi ya “Santa Maria di Monte Santo”. Lakini kwa sababu za migogoro ya kijamii, Provinsi ilitoweka, ndipo hapo konventi za “Carmine Maggiore” zikawekwa tena chini ya mamlaka ya Mkuu wa Shirika isipokuwa toka miaka ya 1910 hadi 1920 zilipokuwa sehemu ya Provinsi ya Neapoli. Mwaka 1947 ikateuliwa Komisarieti ya “La Vergine Bruna” kutokana na konventi za “Carmine Maggiore” na konveti nyingine mbili. Komisarieti Kuu ya “La Vergine Bruna” imewalea vijana Italia kutoka Tanzania toka mwaka 1984. Na mwaka 2009 ilifungua misheni nchini Tanzania. Kwa sasa wako mapadre sita Wakarmeli Watanzania na wanafunzi sita wanaoelelewa nchini mwao Tanzania, Morogoro.