Sehemu ya kwanza
Ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao. ».(Yoh 17: 26)
Kutoka Magisterium ya Kanisa:/ Kutoka Mafundisho ya Kanisa
"Uharaka wa maisha ya leo unasababisha kufungwa milango mingi kwa kutokutana, mara kwa mara kwa kuogopa mingine - milango ya vituo vya ununuzi na uhusiano wa mtandao ndiyo daima hufunguliwa - lakini katika maisha ya wakfu isiwe hivyo: kaka na dada ambao Mungu ananipa ni sehemu ya historia yangu, ni zawadi ya kuhifadhiwa. Isitokee kuangalia skrini ya simu ya mkononi zaidi ya macho ya ndugu, au kujiweka kwenye mipango yetu zaidi ya Bwana [...] Nanyi pia nendeni kinyume na ulimwengu: maisha ya ulimwengu hukataa kwa urahisi umasikini/ufukara, usafi wa moyo na utii, Ninyi ni pambazuko la kudumu la Kanisa Mkusanyike ndani ya Yesu kama kaka na dada, vijana na wazee, ili kuondokana na maneno ya kigumba ya siku za zamani , ile hamu inayoua roho, ili kunyamazisha hali ya ''hapa hakuna kitu kizuri tena'' Ikiwa wanakutana na Yesu kila siku, na ndugu, moyo hauelekezwi siku za nyuma au wakati ujao, lakini anaishi leo ya Mungu kwa amani na wato wote "(Papa Francesco 2.02.18)
Kwa maisha ya kindugu katika jumuiya, mimi nina wasiwasi kwamba kuna taasisi ambazo tamaduni nyingi na kuzifanya za kimataifa ha kuonekani kama utajiri, lakini kama tishio, na wanaziishi kama mgogoro, badala ya kuziishi kama fursa mpya zinazoonyesha uso wa kweli wa Kanisa na wa maisha ya kitawa na ya wakfu. Ninawaomba viongozi wa Taasisi kujifungua kwa njia mpya ya Roho, ambayo inavuta ambapo inataka na jinsi inavyotaka (tazama Yoh 3: 8) na kuandaa kizazi cha tamaduni nyingine kuchukua jukumu hilo. Akina dada, ishini kimataifa katika Taasisi zenu kama habari njema. Ishini mabadiliko ya uso wa jumuiya zenu kwa furaha, na si kama uovu muhimu kwa ajili ya uhifadhi. Umataifa na tamaduni kati ya mataifa usirudi nyuma. (Papa Francis kwa UISG 10.05.19)
Kwa hiyo, mimi natarajia kwamba "Ushirika wa kiroho" ulio olekezwa na Mtakatifu Yohana Paulo II utakuwa uhalisia na kwamba ninyi mko mstari wa mbele katika kupokea " changamoto kubwa iliyo mbele yetu" katika milenia hii mpya: "kulifanya Kanisa nyumba na shule ya ushirika. "Nina hakika kuwa katika mwaka huu mtafanya kazi kwa undani ili wazo la undugu walilolifuata Waanzilishi likue katika viwango tofauti, kama miviringo katika mzunguko. Ushirika hutekelezwa hasa ndani ya jumuiya zenyewe husika za Taasisi. Kwa suala hili, nawaalika msome mara kwa mara mafundisho yangu ambayo sichoki kamwe kuwakosoa kuhusu, uvumi, wivu, husuda, upinzani, ni tabia ambazo hazina haki ya kuishi katika nyumba zetu. Kutokana na nguzo hii, njia ya upendo inayojifungua mbele yetu, ni ile isiyo na mwisho, kwa sababu ni suala la kutafuta kupokeana na kujaliana, kuweka katika matendo ushirika wa mali na wa kiroho, na wa kusahihishana kindugu heshima kwa watu waliodhaifu zaidi ... Ni "fumbo" la kuishi pamoja ", ambalo hufanya maisha yetu kuwa" hija takatifu ". Lazima pia tujiulize kuhusu uhusiano kati ya watu wa tamaduni tofauti, kwa kuzingatia kuwa jumuiya zetu zinazidi kuwa za kimataifa. Jinsi ya kuruhusu kila mtu kujieleza, kukubaliwa na vipaji vyake maalum, kuwa mdau wa kuwajibika pamoja kikamilifu?
(Papa Francis, Mwaka wa Maisha ya wakfu, 21/11/2014)
Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo niliwatuma hao ulimwenguni Yoh 17:18).
Utume wa matifa, unaendelea kuwa muhimu, lakini hatupaswi kupoteza maono ya utaratibu huu mzuri wa utamadunisho ambao hausahau kamwa kuwa Injili inapaswa kuingilia katika tamaduni, kuanzia makundi yenyewe ya kila utamaduni, kwa heshima na bila kulazimisha. Uinjilishaji halisi unatembea njia ya ushuhuda. Nimelisema wakati mwingine: kivutio ndiyo, kulazimisha hapana"(Papa Francis 10.12.18)
Nasubiri bado kutoka kwenu kile ninachowaomba wana Kanisa wote: Kutoka wao wenyewe, kwenda pembezoni halisi. "Nenda ulimwenguni mwote" lilikuwa neno la mwisho ambalo Yesu aliwaeleza watu wake na ambalo anaendelea kutueleza sisi sote leo (angalia Mk 16:15). Kuna watu wote wanaosubiri: watu ambao wamepoteza matumaini yote, familia zenye magumu, watoto waliotelekezwa, vijana wanaokataliwa kesho yao, wagonjwa na wazee walioachwa, matajiri walioshiba mema lakini watupu rohoni, wanaume na wanawake wanaotafutaji maana ya maisha, wenye kiu ya Mungu ... Natarajia kutoka kwenu matendo halisi za kuwapokea wakimbizi, ya ukaribu kwa masikini, ya ubunifu katika katekesi, katika kutangaza Injili, katika kuanzisha maisha ya sala. Kwa hivyo natumaini kuimarisha miundo, matumizi ya nyumba kwa ajili ya kazi ambazo zinajibu mahitaji ya sasa ya uinjilishaji wa upendo, ufanisi wa kazi kwa mahitaji mapya. (Papa Francis, Mwaka wa Maisha Mtakatifu, 11/21/2014)
Umoja, unaweza kukabiliana na ugumu wowote na jukumu la kukutana na ndugu wengine walioko nje, waliotengwa na jamii. Tunaishi utamaduni wa kutengwa, utamaduni wa taka. Tunapaswa kwenda nje kukutana na ndugu hawa waliotengwa, waliachwa katika hatima yao, waliokanyagwa kwa maslahi ya ubinafsi ... Wao pia ni ndugu zetu ambao wanahitaji msaada wetu na haja ya kupata uwepo wa Mungu ambaye huenda kukutana nao. Huko ninyi pia mnatumwa ili kutafsiri roho ya heri katika uhalisia kupitia matendo ya huruma: kwa kusikiliza na kujibu sauti ya wale wanaoomba mkate na haki; kuleta amani na kukuza ushirikiano kwa wale wanaotafuta maisha yenye heshima zaidi; mkifaraji na kutoa sababu za matumaini ya huzuni na mateso ya wanaume na wanawake wengi wa nyakati zetu ... Hii iwe ndio dira inayoongoza njia zenu kama wamisionari ndugu. (Papa Francis anasema "verbiti", 06.22.2018)
Niruhusu kurudia tena: Uhimidiwe, Bwana, kwa kazi hii ya ajabu ya watu wa Amazon na kwa viumbe mbalimbali vyote ambavyo vilivyomo katika nchi hizi, [...] Ninaona ni muhimu kufanya jitihada za kujenga uhai wa kitaasisi wenye heshima, kutambua na kujadiliana na watu wa asili (wenyeji); kuchukua na kukomboa utamaduni, lugha, mila, haki na (maisha ya) kiroho (spiritualità) ambavyo ni vyao wenyewe. Majadiliano ya kiutamaduni ambayo ninyi ni "washiriki muhimu, hasa wakati mnapoendelea na miradi mikubwa inayohusu [nafasi] zenu". Utambuzi na mazungumzo itakuwa njia bora ya kubadilisha mahusiano ya zamani yaliyotokana na kutengwa na ubaguzi. [...] kuna uharibifu mwingine wa maisha unaosababishwa na uchafuzi huu wa mazingira unaosababishwa na uchimbaji haramu. Ninataja usafirishaji wa watu: kazi ya utumwa na unyanyasaji wa kijinsia. Ukatili dhidi ya vijana na dhidi ya wanawake ni kilio kinachopanda mbinguni: "Imeniumiza daima hali ya wale ambao kwa namna mbalimbali wako chini ya aina tofauti za usafirishaji wa binadamu. Ningependa kusikia kilio cha Mungu anapotuuliza sisi sote: "Yuko wapi ndugu yako?" (Mwanzo 4,9). Yu wapi ndugu yako mtumwa? [...] Tusijifanye kana kwamba hakuna kitu na tusiangalie kwingine. Kuna matatizo mengi. Swali ni kwa kila mtu! ». (Mkutano na watu wa Amazon, Hotuba ya Baba Mtakatifu, 19.01.2018)
Baba mtakatifu, kwa jina lako ulilonipa uwalinde hawa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo. (Yoh 17:11)
Msiogope kuwa wachache, badala yake ugopeni kutokuwa na maana, msiogope kuacha kuwa nuru ambayo inawaangazia wale ambao wameingizwa katika "usiku wa giza" wa historia. Msiogope pia "kukiri kwa unyenyekevu, na wakati huo huo kwa ujasiri mkubwa katika Mungu Upendo, udhaifu wenu". Badala yake kuweni na hofu; ya kuacha kuwa chumvi ambayo inatoa ladha kwa maisha ya wanaume na wanawake wa jamii yetu. Wanyenyi kwa ujasiri kuwa watumwa ambao wanatangaza ujio wa asubuhi; kuwa chachu mahali ambapo mtakuwepo na kujikuta hata kama hii inaonekana haina faida halisi na ya haraka kwenu (Papa Francis kwa UISG 10.05.19)
Waanzilishi wetu walijisikia huruma ambayo Yesu alikuwa nayo wakati alipoona umati wa watu kama kondoo wanaotanga tanga bila mchungaji. Kama Yesu, kwa kuongozwa na huruma hii, alitoa neno lake, akaponya wagonjwa, alitoa mkate kula, akajitoa nafsi yake mwenyewe, hivyo pia Waanzilishi walijiweka katika utumishi wa ubinadamu ambao Roho aliwapatia, kwa njia tofauti sana: maombezi, mahubiri ya Injili, katekesi, elimu, huduma kwa masikini, wagonjwa ... ndoto ya upendo haijui mipaka na imeweza kufungua barabara zisizo na idadi za kupeleka pumzi ya Injili katika tamaduni na katika maeneo mbalimbali ya jamii.
(Papa Francis, Mwaka wa Maisha Mtakatifu, 21/11/2014)