Kundi la kwanza la vijana watatu Wakarmeli waliolelewa Tanzania lilianza unovisi 21 Julai, 2018, mara baada ya kumaliza masomo ya falsafa pale Morogoro. Walienda Zimbabwe kwa ajili ya kipindi cha unovisi cha mwaka mmoja kulingana na katiba za Shirika. Vijana hao walikuwa Dickson Richard Sambala, Athanas Mhina Ngassa na Pascal Dominic Mkaka. Waliondoka tarehe 20 Julai, 2018. Walichelewa kwenda kwa sababu walichelewa kumaliza mitihani yao ya chuo. Kwani walitakiwa kuanza unovisi tarehe 6 Julai, 2018 lakini haikuwezekana. Mwalimu wao Fr. Victor Alphonce Biramata, O.Carm na Mkuu wa shirika alijaribu kuwaombea ruhusa chuo lakini ilishindikana. Ndipo alipomwandikia Mkuu wa Shirika Zimbabwe akimwomba waanze unovisi mwishoni mwa mwezi wa saba, ndipo alipokubali na kumwambia kuwa hamna shida. Hii ilikuwa ni mara yao ya kwanza kutoka nje ya Tanzania.
Wanovisi wakiwa na mshauri wa Afrika, Padre Conrad Mtizahepo. 2019.
Wanavisi wakiwa katika picha ya pamoja 2019. Wa kushoto mwa picha ni mnovisi kutoka Zimbabwe. Wengine watatu ni kutoka Tanzania.