Padre Innocent Kaigalula, O.Carm. Huyu ndiye padri wa kwanza mtanzania. Alisoma masomo ya falsafa na teolojia huko Italia katika Jimbo la Napoli. Alipadrishwa tarehe 12.09.1999. Kwa sasa anaishi Italia.
Padre Thomas Mtey, O.Carm. Alipewa Daraja ya Upadre 19.11.2006 na Askofu Filippo Iononne, O.Carm. Alisoma masomo ya falsafa na teolojia huko Italia katika Jimbo Kuu la Napoli. Ni padri wa pili mtanzania katika Shirika la Wakarmel.
Padre Dominic Somola, O.Carm. Alisoma masomo ya falsafa na teolojia huko Italia katika Jimbo Kuu la Napoli. Aliweka nadhiri za daima tarehe 09.01.2008. Akapata Daraja ya Upadri tarehe 24.08.2012.