Hii ndiyo nembo ya Shirika ambayo ina vitu viwili muhimu sana. Kuna alama ya mlima ambao ncha yake inaelekea mbinguni na nyota tatu za dhahabu, moja katikati ya mlima na nyingine mbili zimewekwa kwa ulinganifu hapo juu, moja iko upande wa kushoto na nyingine iko upande wa kulia wa mlima. Ni wazi alama ya mlima inakumbusha mlima Karmeli ulio mwanzo wa Shirika. Yawezekana nyota ya chini inamwakilisha Bikira Maria nyota ya bahari na zile mbili za juu zinawawakilisha Eliya na Elisha. Juu ni mkono wa Eliya akiwa na upanga mkononi mwake akizungukwa na maneno:“Zelo Zelatus Sum pro Domino Deo exercituum” – “Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana, Mungu wa majeshi” (1Fal 19:10). Maneno ambayo yamekuwa ndiyo “Motto” ya Shirika. Habari zaidi kuhusiana na ishara ya upanga; soma 1Fal 18: 25-40 na Ebr 4:12.
“Nimeona wivu mwingi kwa ajili ya Bwana, Mungu wa majeshi”
Nembo ya shirika la Wakarmeli, moja ya upande wa kushoto inatumiwa na O.Carm na ya kulia inatumiwa na O.C.D. Kila Shirika lina kiongozi wake lakini Kanuni ni moja, maisha ya kiroho ni mamoja na utume ni mmoja.
Mabaki ya langu la kuingia katika makazi ya wamonaki Wakarmeli katika Mlima Karmeli