Tuliwasili katika nyumba hii siku ya alhamisi tarehe 6 Oktoba mwaka 2016 majira ya saa tatu asubuhi kuanza safari ya malezi kwa mwaka huu mpya wa masomo 2016-2017. Tuliwasili tukiwa jumla ya watu sita yaani Padre Victor pamoja na wanafunzi wapya wawili, Boniphace pamoja na Felix, na wanafunzi wengine wazoefu watatu, Athanas, Dickson pamoja na Pascal
Baada tu ya kuwasili asubuhi ile tulianza kushusha mizigo tuliyokuja nayo kutoka Dar es Salaam na kuingiza ndani baada ya hapo tulianza kuisafisha nyumba kwani haikuwa kwenye hali nzuri na tulifanikiwa kuisafisha ingawa hatukumaliza yote na kisha kuanza kuweka vitu vya muhimu kama vile jiko ambapo tulikuja na mafundi kutoka Dar res Salaaam amabo walifanikiwa kuweka jiko katika hali yake pamoja na kuunganisha ili lianze kufanya kazi na haikiuchukua muda kazi hiyo ilikamilika kwa kiasi kikubwa baada ya kwenda mjini kuwachukulia vifaa ambavyo vilirahisisha kumaliza kazi yao kwa ufanisi.
Boniphace
Kisha chakula cha mchana kwa mara ya kwanza kilipikwa na tulijumuika wote kwa pamoja mezani mnamo muda wa saa tisa baada ya maandalizi ya hapa na pale kukamilika tulijumuika pamoja mezani pamoja na mafundi tuliokuja nao kutoka Dar es salaam na baada ya chakula taratibu nyingine za usafi pamoja na mafundi tulioambatana nao kurudi Dar es Salaam na kisha mapumziko ya muda mfupi yalifuatia.
Jioni ile tuliingia katika sala za jioni na baada ya sala za jioni tujuimuika tena katika chakula cha jioni na baadae tuliagana kwa ajili ya mapumziko ya siku hiyo. Ijumaa ya tarehe 7 Oktoba 2016 mapema ya saa mbili asubuhi tuliingia katika kipindi cha sala asubuhi kikifuatiwa na chai ya asubuhi na baada ya chai ya asubuhi tuliendelea na kazi ya usafi wa nyumba ambapo siku ya kwanza kazi hii haikukamilika kwani nyumba ilikua chafu na ilikua imejaa vumbi na hivo ilituchukua mud asana kuisafisha kwa nguvu na akili sana na hivyo tulijikuta tukitumia muda mwingi kusafisha nyumba pamoja na mazingira yanayoizunguka nyumba hii
Baada ya kazi hizo za usafi tuliendelea na kipindi cha sala za mchana ambacho kilifuatiwa na chakula cha mchana na kisha wanajumuiya wengine walikwenda mjini kununua vitu, vyakula pamoja vifaa mbalimbali vya kuongezea nguvu katika usafi na baadhi tuliingia katika amapumziko ya muda mfupi. Na baadae waliokwenda mjini walirudi na hivyo ratiba nyingine ziliendelea
Kiufupi nyumba ulikua katika hali nzuri kama tulivyoiacha siku ya kwanza tulipoitembelea kwa mara ya kwanza na hata tuliporudi tuliikuta kwenye hali nzuri zaidi safari hii ilioboreshwa zaidi kwani yale mapungufu ya awali yalirekebishwa ili kuendana na mahitaji yetu ambapo ndani kuna marekebisho kidogo yalifanyika na hata jikoni pia kuna vitu viliongezwa na kwa hakika viliongeza mvuto wa nyumba.
Kiujumla nyumba hii ni nzuri kwani ina kila huduma zote ambazo tunazihitaji kama vile maji, umeme na hata mazingira yake ni mazuri pia kama nilivosema hapo mwanzo kwani yana utulivu wa hali ya juu. Kwa upande wa huduma za kijamii, nyumba hii ipo takribani kilometa tatu kutoka ilipo Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro na mita chache kutoka kilipo chuo cha Jordan ambapo wanafunzi wetu wanasoma Faslsafa hapo chuoni. Nymba hii imepakana na majirani kadhaa na kati ya hao majirani wapo Masista wa Klausula.