Utawa wa Tatu wa Walei
Utawa wa Tatu walei
Kiunganishi cha msingi cha mtawa wa tatu na Karmeli ni nadhiri za ahadi. Wajibu huu hujionesha kwa kwa aina fulani ya ahadi, au katika nafasi nyingine, kama ilivyo desturi yetu ya kale, kwa kuweka viapo vya utii na usafi wa moyo kwa mujibu wa majukumu ya hali yao. Kwa njia hii, mtawa wa tatu hujiweka wakfu kwa Mungu kwa undani zaidi ili aweze kumpa ibada yenye uzito zaidi. Kwa nadhiri kiukweli mtawa wa tatu hukusudia kuzingatia ahadi za ubatizo za kumpenda Mungu zaidi ya yote na kumkataa shetani na hila zake zote. Uhalisi wa nadhiri hizi u katika njia zinazochaguliwa ili kufikia ulingano kamili wa Kristo.
Kundi la wamisionari wakarmeli la Vico Equense Italia
Utawa wa tatu wa wakarmeli ni walei ambao hufanya hadharani nadhiri za ahadi za kuishi njia ya maisha ya wakarmeli. Hufanya hivyo kwa kupokea skapulari ya karmeli. Huishi kulingana na karama za shirika na kuweka vitendoni mashauri ya kiingili ya usafi wa moyo na utii kulingana na hali zao.
Wana Utawa wa Tatu
Neno 'Utawa wa Tatu' si neno linalotumika kwa utaratibu wa kihierarkia, au neno linalotumika kuonesha kwamba wito wa walei Warmeli si muhimu kama wito wa 'Utawa wa Kwanza'. Badala yake ni kuwa neno hili ni la kihistoria tu. Makundi mbalimbali yalikuwa yanazaliwa na kukua kwa nyakati tofauti. Kundi la kwanza kuzaliwa au kuwepo ndilo linaloitwa Utawa wa Kwanza. Hili ndilo lile kundi la wakrmeli waeremiti walioishi mlima Karmeli wakiwa ndugu (brothers) -watawa mapadre na watawa wasio mapadre. Kundi la Pili kutokea katika Karmeli linaitwa Utawa wa Pili. Hawa ndio wale wanaoishi maisha ya faragha yaani wamonaki wa kike (Nuns). Na kundi la tatu kuwepo au kuzaliwa katika Karmeli ndilo linaloitwa Utawa wa Tatu. Likiwa na maana ya masista na walei. Utawa wa Tatu wa masista wanajishughulisha na maisha ya kitawa wakiwa na maisha ya kikanuni na kitume. Wanaishi katika jumuiya na kufanya utume duniani moja kwa moja. Utawa wa Tatu wa walei unawahusu wale waamini wa kawaida na baadhi ya mapadre wa majimbo ambao hufuata njia ya Karmeli ya maisha katika mazingira yao wenyewe, baada ya kuweka ahadi na kupokea skapulari ya Karmeli.
Signora Flavia Fascia Lamantia aliyechora Kanisa linalotarajiwa kujengwa bunju akiwa na mwanae Emmanueli. Picha hii ilipingwa ndani ya Basilica la Karmeli kule Napoli Italia.
Neno 'Utawa wa Tatu' maana yake nini? Neno 'Utawa wa Tatu' si neno la kihierarkia, au dalili za kuonesha kwamba wito wa walei wa Karmeli si muhimu kama wa 'Utawa wa kwanza' wa Ndugu. Neno hili linatumika ili kuonesha mpangilio wa kihistoria ambamo makundi mbalimbali yalizaliwa ndani ya shirika. Baada ya kundi la awali Wakarmeli waeremiti (hermits) walijiunda kama Ndugu wa Utawa wa Kwanza. (ambao baadhi yao ni makuhani/makasisi). Utawa wa pili ni watawa kike wamonaki Utawa wa Tatu umegawanyika katika sehemu mbili masista wa maisha ya kitume na walei wenye maisha ya familia au hata mapadre wa jimbo wanaopokea skapulari kwa ibada na roho ya kikarmeli wakiwa wamefanya nadhiri za ahadi. Hawa wanafuata njia ya maisha ya Karmeli katika mazingira yao wenyewe, wanakofanyia kazi.
Walei wakarmeli hutoka sehemu mbalimba wengine wakiwa ni wanataalamu. Baada ya kupokelewa ndani ya shirika wanaendelea kuishi nyumbani kwao na kufanya kazi za kilimwengu, wakionesha upendo wao wa Mungu kwa njia ya upendo wa familia zao, na kwa majirani zao.
Maisha ya kikarmeli kwa mlei ni kuishi katika roho ya umoja wa kweli na familia nzima ya Karmeli ambamo ndani mwake tumekubalika kikamilifu na kuingizwa.