Abramu -Ibrahimu -Baba wa imani
1. Majina yake: [Abramu-Ibrahimu]
(a) Abramu - jina la awali la Ibrahimu [Baba mwinuliwa]
(b) Ibrahimu –jina la pili Abramu [Baba wa mataifa, baba wa wengi [Mwa 17:5]. Alikuwa ni mtoto wa Tera (Mwa 11:26). Mkewe alikuwa ni Sarai [Malkia] (Mwa 11:29). Akiwa na umri wa miaka sabini alikuwa akiishi katika nchi ya Uru ya Wakaldayo (Mwa 11:28). Baadaye walihamia Harani (Mwa 11:31) [Itafsiriwa kama mwito (Mdo 7:2-4)].
2. Mwito wa Abramu – “Toka nenda” -Nchi ya ahadi [Mwa 12:1]
(a) Ahadi ya kwanza: itakuwa taifa kubwa na mbaraka wa mataifa
Abramu akiwa Harani alipokea mwito kutoka kwa Mungu [Mwa 12:1-3; Yos 24:3]. Alipokea ahadi ya kuwa taifa kuwa (Mwa 12:2) [inakuja kukamilishwa nyakati za Daudi na Sulemani], naye akajiaminisha kwa Mungu bila kujua aendako [Ebr 11:8]. Alijiaminisha kwa yule aliyekuwa amemwita.
3. Abramu –anaitikia mwito wa Mungu [Mwa 12:4-5a].
(b) Ahadi ya pili: anaahidiwa yeye na uzao wake kuwa watapewa nchi [Mwa 12:7]
(c) Ahadi zote mbili zinarudiwa tena: [Mwa 13:15-16]
4. Anaacha jamaa zake, nchi yake na utajiri na kuanza maisha ya kuhamahama
Alikuwa akiishi katika vibanda. Aliweka makazi yake ya kwanza katika nchi ya Kanaani pale Shekemu, (12:6), akaenda kuishi maeneo ya Betheli (12:8) mahali alipojenga altare, akazidi kusogea kusini. Hatimaye akaingia Misri kwa sababu ya njaa (Mwa 12:10-20).
5. Abramu anarejea kutoka Misri
Akarejea tena Betheli -Kanaani akiwa na utajiri (Mwa 13:2). Akaishi kwenye mialoni ya mamre (Mwa 13:18).
6. Abramu na Lutu
Abramu alikwenda kumkomboa Lutu nduguye aliyekuwa ametekwa na mfalme Kedorlaoma na wafalme wengine. Alipokuwa akirejea kutoka kumkomboa Lutu na mali zilizokuwa zimetekwa alipitia Salemu (Yerusalemu) akakutana na Melkizedeki mfalme wa Salemu, Kuhani wa Mungu aliye Juu sana. Akampatia 10% ya mali yake (Mwa 14:18-20).
Ibrahimu alioa mke mwingine jina lake Ketura. (Mwanzo 25:1). Alikufa akiwa na umri wa miaka 175. (Mwanzo 25:7).
7. Mungu na Abramu –Ahadi na Agano [Mwa 15:1-21] -[Agano –kutahiri 17:11; Lk 2:21]
Uzao wake utakuwa kama nyota za mbinguni na atairithi nchi ya Kanaani. Ahadi hiyo inadhibitishwa kwa sadaka za kuteketezwa kati ya Abramu na Mungu.