Askofu na mtunga sheria wa Shirika letu la Wakarmeli
Mwanzo Yos 1:8
Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo.
Sala
Tuombe
Ee Mungu, uliyependekeza kwetu kwa njia ya Mtakatifu Albert kanuni ya maisha ya kiinjili kwa ajili ya kutuongoza katika njia ya upendo mkamilifu, uijalie familia yako kuishi wakati wote katika utii kwa Yesu Kristo na kumtumikia kwa uaminifu mpaka kifo. Tunaomba hayo kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo Mwanao, anayeishi na kutawala pamona nawe, katika umoja wa Roho Mtakatifu, Mungu, daima na milele. Amina.
Somo la kwanza Efe 6:10-18
Somo la Waraka wa Mtume Paulo kwa Waefeso
Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake. Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama. Basi simameni, hali mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.
Neno la Bwana
Wimbo wa katikati Zab 119
Kiitikizano: Neno lako ni taa ya miguu yangu,
Na mwanga wa njia yangu. K
Sheria yako naipenda mno ajabu,
Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa. K
Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya,
Ili nilitii neno lako.
Sikujiepusha na hukumu zako,
Maana Wewe mwenyewe umenifundisha. K
Mausia yako ni matamu sana kwangu,
Kupita asali kinywani mwangu.
Neno lako ni taa ya miguu yangu,
Na mwanga wa njia yangu. K
Shuhuda zako nimezifanya urithi wa milele,
Maana ndizo changamko la moyo wangu.
Mimi ni mtumishi wako, unifahamishe,
Nipate kuzijua shuhuda zako. K
Shuhuda zako ni za ajabu,
Ndiyo maana roho yangu imezishika.
Kufafanusha maneno yako kwatia nuru,
Na kumfahamisha mjinga. K
Shangilio Kol 3:16a.17
Alleluya, alleluya
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu,
Na kila mfanyalo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu.
Alleluya
Injili Mt. 20:25-28
Somo la Injili Takatifu, ilivyoandikwa na Mathayo
Lakini Yesu akawaita, akasema, Mwajua ya kuwa wakuu wa Mataifa huwatawala kwa nguvu, na wakubwa wao huwatumikisha. Lakini haitakuwa hivyo kwenu; bali mtu ye yote anayetaka kuwa mkubwa kwenu, na awe mtumishi wenu; na mtu ye yote anayetaka kuwa wa kwanza kwenu na awe mtumwa wenu; kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa nafsi yake iwe fidia ya wengi.
Neno la Bwana
Kuombea dhabihu
Ee baba, kwa wema wako mkubwa ametuchagua sisi kuwa mashuhuda na watangazaji wa upendo wako, upokee matoleo ya mkate na divai na utufanye tuwe walinzi waaminifu wa neno lako. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo, Bwana wetu.
Amina.
Utangulizi wa wachungaji
Komunyo Mt. 23:10.8
Sala baada ya kumonyo
Tuombe
Kwa nguvu ya sakramenti hii na kupitia maombezi ya Mtakatifu Albert tunakuomba, Bwana: turuhusu tuishi katika uwepo wako, ili, tunapoitafakari sheria yako mchana na usiku, na tukeshe katika kuomba, tunastahili kukufikia wewe katika heri ya utukufu. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo, Bwana wetu. Amina.
Baraka