YOHANE WA MSALABA
KIONGOZI WA KUMTAFUTA MUNGU
Mmistiko, Mshairi, Padre na Mwalimu wa Kanisa
“Mwisho wa maisha yako kipimo cha hukumu kitakuwa juu ya upendo”(Yohana wa msalaba)
Maisha yake
Alizaliwa tarehe 24.06.1542 –akiwa na jina la asili la Juan de Yepes y Alvarez huko Fontiveros Avila Hispania. Baba yake alikuwa maskini na alifariki Yohane akiwa bado mdogo. Hivyo mama yake alichukua jukumu la kumlea. Waliishi kwa kuhamahama wakitafuta kazi. Ni katika kipindi hicho Yohane alijifunza kujitoa sadaka. Ni katika umaskini huo na mates ohayo Yohane alijifunza kutafuta furaha si katika mambo ya dunia, bali katika Mungu.
Shule
Alisoma Medina del Campo. Akiwa na miaka 14 alipata kazi ya kuwahudumia wagongwa hospitalini. Alisoma shule ya Majesuit.
Katika Karmeli
Aliingia Karmeli tarehe 24. 02. 1563 na kupata vazi la shirika na kuchagua jina la Juan de santo Matia –Yohane wa Mt. Matthias. Alisoma Chuo kikuu cha Salamanca ambapo alianza kufundisha angali bado mwanafunzi.
Upadrisho
Alipata Daraja Takatifu ya Upadre mwaka 1567. Baada ya hapo alikutana na Mt. Teresa wa Yesu. Akiwa Karmeli aliombwa na Mt. Teresa wa Avila kufanya mabadiliko ndani ya shirika ili kulirudisha shirika kwenye kiini chake cha sala.
Kazi hiyo aliifanya huko Duruelo ambako alibadilisha jina toka Yohane wa Mt. Matthias na kuwa Yohane wa msalaba.
Lakini watawa wenzake waliliona wazo hilo kuwa ni hatari, wakamteka mwaka 1577 na kumfungia kwenye chumba. Alikuwa akipingwa na watawa wenzake. Katika chumba hicho upendo wake ulizi na kuwa kama moto. Hakuwa amebakiwa na kitu chochote isipokuwa Mungu. Alipata faraja kutokana na imani hiyo. Alifanikiwa kutoroka mwaka 1578. Alifanikiwa kuondoka na mashairi yake aliyoyaandika alipokuwa amefungwa. Tangu kipindi kile alianza kushirikisha upendo wake wa Mungu.
Aliwahi kuwa vika wa provinsi ya Andalusia toka mwaka 1585 hadi 1587.
Kazi zake
Mwalimu wa sala na mwongozaji wa roho kuelekea kwenye muungano na Mungu. Aliyaelewa Maandiko Matakatifu kwa kina. Alisisitiza sana juu ya Neno wa Mungu aliyetamkwa katika ukimya.
· Kupanda Mlima Karmeli (Ascent of Mount Carmel)
· Usiku wa giza wa nafsi (Dark night of the soul)
· Wimbo wa kiroho wa nafsi (The Spiritual Canticle of the soul)
Kifo chake
Alifariki dunia tarehe 14.12.1591 huko Ubeda, Andalusia.
Kutangazwa Mtakatifu
Alitangazwa mwenye heri tarehe 25.01.1675 na Papa Klementi X na alitangazwa Mtakatifu tarehe 27.12. 1726 na Papa Benedikt XIII.