MT. TERESA WA AVILA
MTAKATIFU TERESA WA AVILA –TERESA WA YESU MMONAKI WA KIKE MKARMELI, MMISTIKO NA MWALIMU WA KANISA
Mt. Teresa alizaliwa 28.03.1515 huko Avila Hispania katika familia ya watu 10. Tangu akiwa mtoto alikuwa akivutiwa sana na maisha ya watakatifu. Alikuwa mtoto wa Don Alfonso mtoto wa Toledo mfanya biashara. Baba yake alioa mara mbili. Mke wa kwanza aliitwa Dona Catalina del Peso y Hefiao. Alizaa naye watoto watatu. Mke wa pili alikuwa Dona Beatriz Davila y Ahumada aliyezaa watoto tisa. Teresa alikuwa mtoto wa watatu katika familia ya Don Alfonso kwa mke wa pili. Mama yake alifariki wakati Teresa akiwa na umri wa miaka 12. Baada ya msiba huo Teresa alikabidhiwa kwa wamonaki waagostini mwaka 1531. Akiwa bado mdogo alisoma maisha ya mashahidi wengi ambao walimvutia na akawa anatamani kuwa shahidi. Alikuwa anasema anataka kumwona Mungu.
Baada ya kusoma barua ya Mt. Yoremu Mt. Teresa aliamua kujiunga na maisha ya utawa.
Aligundua kuwa vitu vyote vya dunia hii vitapita.
Mungu peke yake ndiyo kila kitu. Ukweli huu utakuja kuonekana na katika shairi lake.
“Let nothing disturb you, let nothing frighten you, All things are passing away: God never changes. Patience obtains all things. Whoever has God lacks nothing: God alone suffices”.
Kuingia Karmeli
Mwaka 1535 akiwa na umri wa miaka 20 alijiunga na wamonaki wa Shirika la Wakarmeli kwenye monasteri ya umwilisho. Akachukua jina la Teresa wa Yesu. Baada ya miaka 3 alikuwa ndani ya monasteri akiwa mgonjwa. Aliwahi kuandika hivi “nilitamani kuishi lakini niliona wazi wazi kuwa sikuwa naishi bali nilikuwa napambana na uvuli wa mauti”. Alipenda kusali na kutafakari sana. Alihitaji utulivu wa kutosha. Alihangaika sana kuingia ndani mwake. Baada ya kuona ni mdhaifu, aliwageukia watakatifu waliofanya toba ya kweli Mt. Maria Magdalena na Mt. Agostino.
Mwaka 1543 alipoteza ndugu zake wengi na baba yake pia.
Katika maisha yake kuna tukio ambalo yeye analiita kuwa ndio ulikuwa mwanzo wa kuongoka kwake. Anasema kuwa mwaka 1554 wakati wa Kwaresima alikuwa akiingia kwenye kikanisa cha monastery yao ambapo aliiona picha ya Yesu ambayo ilikuwa imeletwa kwa ajili ya maadhimisho yaliyokuwa yakifanyika katika monastery yao. Yesu alikuwa na majereha makubwa mno na ya ajabu. Tukio hilo lilimgusa sana kwani aliona jinsi Yesu alivyoteseka kwa ajili yetu. Tangu wakati huo maisha yake yalibadilika.
Teresa mgonjwa
Mwaka 1555 alianza kuumwa tena na akaenda kuishi na mwanamke mmoja aliyeitwa Dona Guiomar (mjane) ambaye alikuwa rafiki yake. Alikaa huko kwa miaka mitatu --1555-1558. Aliendelea kuwa na maono kati ya mwaka 1559 na 1560. Alijitahidi kuitafuta njia ya ukamilifu. Moja ya maono yake inasemakana alifanikiwa kuona kuzimu. Akaanza juhudi za kuwasaidia watu ili wasifike huko.
Hatua alizozichukua
Yeye mwenyewe kuishi kikamilifu wito wake
Kujitenga moja kwa moja na mambo ya kidunia
Kuzingatia kwa nguvu zote maelekezo ya Kanuni ya Shirika
Mang’amuzi ya kufanya mabadiliko
Aliamini kuwa Kanuni ilikuwa haifuatwi kama ilivyotakiwa
Aliamini kuwa Kanuni iliyofanyiwa mabadiliko ilikuwa haikidhi kile alichokitamani moyoni mwake. Aliamini kuna Kanuni ya «zamani».
Alitamani kuleta mabadiliko katika monasteri za kikarmeli kama ilivyokuwa kwa Wadominikani.
Mabadiliko -OCD
Alipanga kujenga monastery ambayo ilibidi iwe na watu 13 tu.
Teresa mwanzo aliungwa mkono na mkuu wa Provinsi lakini baada ya kupata upinzani aliamua kujiondoa. Lakini Teresa aliendelea na mpango wake huo.
Maisha ya sala
Aliwahi kusema hivi “Maombi/sala ni tendo la upendo, maneno hayahitajiki. Hata kama ugonjwa unavuruga mawazo, katika vyote kinacho takiwa ni utayari wa kupendo.”
Teresa alitaka maisha ya sala yawe ya ukimya sana kama ilivyokuwa Mlima Karmeli.
Alitaka wamonaki waishi maisha ya
· Sala ya ukimya na sala muungano
· Upweke
· Tafakari
· Maisha ya ufukara
· Kutokula nyama siku zote
Kazi zake
Interior Castle (mansions)–ngome ya ndani
“Nilianza kufikiria nafsi kana kwamba ni ngome iliyotengenezwa kwa almasi”
Katika maono yake ya kiroho aliiona roho kwa ujumla wake kama ngome ya kioo yenye makao saba, ambayo yeye aliyatafsiri kama safari ya imani kwa njia ya hatua saba inayoishia kuwa na muungano na Mungu. Ngome hii imegawanywa katika makazi saba. Sehemu ya kuishi. Kila hatua inaeleza jinsi ya kumkaribia Mungu. Mlango wa kuingia katika ngome hii ni sala na tafakari.
1. Chumba cha kwa huanza kwa hali ya neema. Lakini roho bado imezungukwa na dhambi. Ndipo hapo huanza kumtafuta Mungu kwa unyenyekevu ili kufikia ukamilifu.
2. Chumba cha pili roho hutafuta kusonga mbele kwa huingia kwa njia ya sala na tafakari -kujitambua. Kuwaza kila siku juu ya Mungu. Kwa kutambua kazi ya Mungu katika nafsi.
3. Chumba cha tatu ni kwa kazi ya neema ya Mungu ambayo huifanya roho kutopenda au kutoinamia dhambi na hivyo roho huvutwa kumpende Mungu zaidi na kutamani kutenda matendo ya upendo -kujitawala.
4. Chumba cha nne ni kwa njia ya sala ya tafakari –(contemplative prayer) –kiwangu cha juu –kujaribiwa na dhambi. Husonga mbele kwa msaada wa neema.
5. Chumba cha tano roho i wazi kupokea zawadi za kimungu. Roho inaamini kabisa mapenzi ya Mungu. Hana shida juu ya vionjo vyake.
6. Chumba cha wanaopenda Roho na Mungu. Roho hutumia muda mwingi kukaa na Mungu. Kutamani kuungana naye. Kuna mateso mengi. Watu hawawezi kukuelewa.
7. Roho inafikia uwazi katika sala na ndoa ya kiroho na Mungu. Kuna utulivu mkubwa, upendo mkubwa, imani kubwa sana.
· Njia ya ukamilifu « The Way of Perfection». Hii ilikuwa kwa ajili ya uongozi maalum wa watawa wake, na kuweka misingi kwa ajili ya kuwajenga zaidi. Sala, ukimya na tafakari.
Upendo wa kindugu
Kujiondoa kwenye vitu vilivyoumbwa –detachment
Unyenyekevu wa kweli.
Ugumu wa kupata padre wa kiroho
Monasteri za kiume –Yohane wa Msalaba
Alitaka hata Wakarmeli wa kiume nao wafanye mabadiliko. Alijua kuwa watakuwa msaada kwa wamonaki wa kike. Ili kutimiza lengo lake hilo aliomba kwa wakuu wa Shirika na wakakubaliana kuwa zitengwe nyumba mbili kwa ajili ya maisha hayo.
Kifo chake
Alifariki tarehe 4 Oktoba 1582 . Siku iliyofuata tarehe 5 Octoba , kama ilivyotokea, kalenda ya Gregory ilianza kutumika. Kutokana na mabadiliko yaliyofanyika ililazimika 5 Oktoba ihesabiwe kama Oktoba 15, na tarehe hii ilipita na ndiyo sikukuu ya Mt. Teresa wa Avila.
Kutangazwa Mwenye heri, Mtakatifu na Mwalimu wa Kanisa
Mt. Teresa alitangazwa mwenye heri tarehe 24. 04. 1614 na Papa Paulo V na alitangazwa Mtakatifu tarehe 12.03.1622 na Papa Gregory wa XV. Alitangazwa kuwa mwalimu wa Kanisa tarehe 27.09.1970 na Papa Paulo VI.isa ya Mt. Teresa wa Avila