Lectio divina ni kulisoma kwa usikivu Neno la Mungu, kulitafakari kama anavyosema Mzaburi "kufafanusha maneno yako kwatia nuru, na kumfahamisha mjinga", na kulisali. Ni njia maalum ya kumwelekea Mungu kwa kulifahamu zaidi Neno lake. Neno la Mungu ni taa na njia "Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga wa njia yangu" (Zab 119:105). Inabidi kulisoma mara kwa mara Neno na kwa njia thabiti. Inabidi moyo upendo kukutana na Mungu. Inabidi kulisoma ili upate kuamini na kumpendeza Mungu. Inabidi kufanya Lectio Divina kwa moyo wote bila kuchoka. Inabidi Lectio iyabadili maisha yako na kukupeleka kwenye ukamilifu. Ukweli ambao unaupata katika kulisoma Neno la Mungu inabidi likulete kwenye sala na tafakari. Neno la Mungu linakusaidia uweze kujua njia gani ya kutembea. Ni mwanga na nuru katika kazi la maisha. Neno la Mungu linagusa historia ya maisha yako yote. Neno la Mungu ni hekima kwa mwanadamu. Lectio divina ni somo la Neno la Mungu linalofanywa katika hali ya sala na tafakari na kuelekea kuijua "siri ambayo tangu zamani zote ilisitirika katika Mungu aliyeviumba vitu vyote" (Efe 3:9).
Maandalizi
Eneo au mahali
Kwa kuwa Lectio divina ni zoezi la tafakari na sala hivyo linahitajika lifanyike sehemu tulivu zinazosaidia tafakari na sala ili washiriki waweze kujikusanya vizuri.
Wakati
Inabidi ifanyike wakati ambao washiriki hawana mawazo juu ya majukumu yao ya kitume na usiwe wakati ambao wamechoka. Uwe wakati mzuri unaomfanya mtu awe huru zaidi katika kusoma Neno la Mungu.
Muda
Inabidi uwe muda mzuri na wa kutosha ili kuwawezesha wote wanaoshiriki wapate muda wa kutosha.
Kiongozi
Inabidi awepo kiongozi atakaye andaa kwa makini somo na kuongoza wengine kufanya tafakari ya kindugu.
Washiriki
Lectio divina ni kwa ajili ya wote, watu wa rika na tabaka mbalimbali. Vema wote wakafika kabla ya kuanza somo na mtu asiondoke kabla ya hitimisho la pamoja.
Tabia -Mwenendo
Tabia yetu inabidi ya unyenyekevu. Kutotanguliza elimu na ufahamu wetu. Tuache Neno lenyewe liongee.
Imani
Biblia Takatifu
Inabidi kuanza kipengele cha kusoma.
Msaada wa vitabu vingine
Katika Lectio unaweza kutumia msaada mwingine kama vile Maoni ya baba wa Kanisa, maoni ya wataalamu wa Maandiko Matakatifu, vitabu vya maandiko ya kiroho na ulinganifu wa Biblia. Lengo la kutumia msaada huo ni kuielewa vizuri Biblia.
Biblia
Inabidi Biblia iwekwe mbele ya washiriki na kupewa nafasi muhimu ili itukumbushe Neno linalo tafakariwa.
Picha -Ikoni
Unaweza kuweka picha itakayo saidia kuwaingiza wanaoshiriki katika tafakari ya fumbo.
Mishumaa
Mshumaa uashwe ishara ya ufufuko wa Bwana (Yoh 8:12).