Sehemu hii inaitwa Injili ya kwanza, habari njema za kwanza. Mungu anatangaza ukombozi wa mwanadamu kutoka katika mikono ya shetani.
Abramu aliahidiwa mtoto [Mwa 15:2-4], [Mwa 17:15-16], [Mwa18:10], kuwa atakuwa baba wa mataifa mengi mwenye uzao mwingi, [Mwa 12:2; 17:5], kama nyota za mbinguni [Mwa 15:5-6], na aliahidiwa nchi kwa Agano [Mwa 12:7; 15:18], na aliahidiwa kuwa atakuwa chimbuko la mbaraka kwa mataifa yote [Mwa 12:3], [Mwa 22:16-18]. Kwa kuwa Ibrahimu aliamini, basi alihesabiwa haki [Mwa 15:6], Kwa sababu Ibrahimu alimtii Mungu kwa kuyasadiki maneno yake [Mwa 26:5].
«Mungu akamwambia Ibrahimu, “Nawe ulishike agano langu, wewe na uzao wako kwa vizazi vyao baada yako. Hili ndilo agano langu utakalolishika, kati ya mimi na wewe, na uzao wako baada yako: Kila mwanamume wa kwenu atatahiriwa. Mtatahiriwa nyama ya magovi yenu, na jambo hilo litakuwa ishara ya agano kati ya mimi na ninyi. Mtoto wa siku nane.....agano langu litakuwa katika mwili wenu, kuwa agano la milele”» [Mwa 17:9-13]. Kwa maagano hayo, baraka za Mungu zingeyafikia mataifa yote. Yesu naye alitahiriwa [Lk 2:21].
Mungu anazirudia ahadi zake alizomwahidia Ibrahimu, sasa anamwahidi Isaka nchi [Mwa 26:3-4], uzao mwingi kama nyota za mbinguni [Mwa 26:4] na baraka kwa mataifa kupitia yeye [Mwa 26:4]. Huyu ni mtoto wa ahadi [Rum 9:7].
5 Ahadi kwa Yakobo [Mwa 28:13-14] –Israeli [Mwa 33:28]
Mungu anamwahidi Yakobo kuwa kwake utatoka uzao mwingi [Mwa 28:14], anamwahidi nchi [Mwa 28: 13] na anamwambia kuwa atakuwa mbaraka kwa mataifa mengi ya dunia [Mwa 28:14].
Yakobo alikutana na malaika Mwanzo 32:1
1. Reubeni, 2. Simeoni, 3. Lawi, 4. Yuda, 5. Dani, 6. Naftali, 7. Gadi, 8. Asheri, 9. Isakari, 10. Zabuloni, 11. Benyamini, 12. Yusufu. Hawa pamoja na familia zao ndiyo mababa wa makabila kumi na mawili ya Israeli.
Kitu gani kilichotokea?
9. Isaka alikuwa na watoto wawili Esau na Yakobo ambao walikuwa ni mapacha [Mwa 25:24-26].
10. Yakobo - Israeli ndiye mababa wa watoto kumi na wawili ambao ndiyo mababa wa makabila kumi na mawili ya Israeli [Mwa 29:31-30:22], [Mwa 35:18].
11. Mungu aliliteua Israeli kuwa Taifa Teule na kufanya nao Agano [Kumb 7:6], [Kumb 28:9], [Kumb 26:19]. Utimilifu wa ahadi kwa Ibrahimu, Isaka na Yokobo [Kumb 29:13].
Baada ya mababu wa Israeli, Mungu aliliunda Taifa Teule la Israeli kama taifa la kikuhani miongoni mwa mataifa yote ni ikiwa ni maandalizi ya kuja kuwaita mataifa mengi kuwa watu wa Mungu. Alianza kutimiza ahadi zake kwa kuwatoa utumwani Misri -Pasaka, akafanya nao Agano katika mlima Sinai [Kut 19:1-24] na hatimaye akawapa zawadi ya Sheria (Torati) kwa mkono wa Musa [Kut 20:1-21].
Uhusiano maalum kabisa kati ya Israeli na Mungu ulijengwa juu ya Agano na Torati. Torati ilikuwa ni uhakika wa wokovu. Kuishika Torati ilikuwa ni kuokoka. Vile vile uhusiano kati ya Israeli na Mungu ulijengwa katika 1. Uwana, Israeli imefanywa kama mwana wa Mungu [Kut 4:22], [Kumb 14:1], [Hos 11:1]. 2. Kujionesha kwa Mungu kwao, [Kut 16:10], [Kut 40:34], [1Fal 8:10-11], 3. maagano [Mwa 15:18], [Kut 24:7-8], [YbS 44:12], 4. Torati –amri za Mungu [Kut 20:1-17], [Kumb 5:1-22], 5. Ibada ya Mungu katika hekalu [], 6. Ahadi kwa mababu (Ibrahimu) [Mwa 12:2], [Mwa 21:12], kwa Musa [Kumb 18:18-19], kwa Daudi [2Sam 7:11-16]. Mungu anaahidi kumjengea Daudi nyumba, itatawala milele 2Sam 7:12-16. Huu ni uaguzi wa Masiya, mwana wa Daudi [Is 7:14; Mik 5:1; Hag 2:23], ambapo Matendo inasema kuwa uaguzi huo ulikuwa wa Kristo [Mdo 2:30].
Masiya kwa njia ya imani [Gal 3:6-9]
«Katika mababu alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele, Amina. Si kana kwamba neno la Mungu limetanguliwa. Maana hawawi wote Waisraeli walio wa uzao wa Israeli. Wala hawawi wote wana kwa kuwa wazao wa Ibrahimu, bali kwa imani [Rum 9:5-9]. «Kama vile Ibrahimu alivyomwamini Mungu akahesabiwa haki. Fahamuni basi, ya kuwa wale walio na imani, hao ndio wana wa Ibrahimu. Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa. Basi hao walio na imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani» [Gal 3:6-9].
«Basi ahadi zilinenwa kwa Ibrahimu na kwa mzao wake. Hasemi “Kwa wazao”, kana kwamba ni wengi, bali kana kwamba ni mmoja, Kwa wazao wako, yaani Kristo» [Gal 3:16]. «Torati imekuwa kiongozi wa kutuleta kwa Kristo ili tuhesabiwe haki kwa imani» [Gal 3,].