Naitwa Felix Malimi, mzaliwa wa Jimbo Katoliki la Kahama Parokia ya Ekaristi Takatifu Kabuhima. Nilizaliwa tarehe 5/09/1992, nikiwa mtoto wa tatu katika familia yetu yenye watoto sita , wavulana tukiwa watatu na wasichana watatu.
Nilipata elimu ya msingi katika shule ya msingi ya uyovu iliyopo katika mkoa wa Geita wilaya ya bukombe na kuhitimu mwaka 2007. Niliendelea na elimu ya sekondari katika shule ya Runzewe ambapo nilihitimu mnamo mwaka 2011 nikiwa na ufaulu wa daraja la nne na point 28 sikuweza kuendelea na kidato cha tano.
Mnamo mwaka 2013 nilirudia kufanya mitihani ya kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Twitange iliyopo katika mkoa wa Mwanza wilaya Sengerema na kufanikiwa kufaulu kwa daraja la Pili. Niliendelea na elimu ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Galano iliyopo mkoani Tanga na kuhitimu mnamo mwaka 2016 na kupata ufaulu wa daraja la kwanza. Baada kuhitimu kidato cha sita nilijiunga na jeshi la kujenga taifa kwa mujibu wa shiria katika kambi ya KJ821 BULOMBORA KIGOMA
Nikiwa katika elimu ya msingi nilipenda sana kutumikia kanisani,nilipenda sana kujitolea kwa ajili ya kumtumikia Mungu hivyo niliendelea na kutumikia na nia yangu ilikuwa kumtumikia milele. Hivyo nilitamani sana kujiunga na seminari lakini sikuweza kupata nafasi ya kujiunga na seminari kutokana na sababu za hapa na pale.
Nikiwa katika elimu ya sekondari nilitiwa moyo na kupata hamasa kutoka kwa mapadri waliokua wanatutembelea katika shule yetu. Waliweza kutupa mwongozo na namna ya kujiunga katika mashirika mbalimbali ya maisha ya wakfu kwa lengo la kumtumikia Mungu kwa njia ya upadri. Kabla ya kutuma maombi katika mashirika mbalimbali niliomba ushauri kutoka kwa dada yangu ambaye ni sista. Aliweza kunisaidia kwa kunieleza juu ya Shirika la Wakarmeli na alinipatia namba ya padre Victor ili aweze kunipatia maelezo zaidi jinsi ya kujiunga na sifa za kujiunga. Baada ya kuongea na Fr. Victor alinikubalia na akaniambia nitume maombi. Siku hiyo nilifurahi na nikatuma maombi ya kujiunga katika Shirika la Wakarmeli. Hatimaye mnamo tarehe 08/09/2016 baada ya kutoka jeshini nikaenda kuanza malezi bunju. Ninamshukuru Mungu kwa hii nafasi aliyonipatia. Naomba mnisindikiza kwa sala na majitoleo yenu katika kuitikia .