Roho ya Wakarmeli ni hamu moto moto ya nafsi ya kutaka kuwa na uzoefu wa moja kwa moja wa Mungu, kukutana naye rohoni . Kwa maneno mengine, roho ya Wakarmeli i katikati ya roho wa maombi, anayeeleweka kama rafiki wa upendo kati ya nafsi ya mtu na Mungu, ambaye hujizamisha katika tafakari kama zawadi ya bure ya Mungu. Roho ya Wakarmeli inalenga kukuza uhusino makini kati ya mtu na Yesu Kristo. Huu ndio mvuto ambao Wakarmeli wameuona na kuutamani kwa Bikira Maria na nabii Eliya. Hawa wawili walikutana na Mungu rohoni mwao, katika upweke na utii wa sauti ya Mungu.
Vyanzo vikuu ya Roho ya Wakarmeli (Carmelite Spirituality):
Vilivyoandikwa:
Kanuni ya Mt Albert wa Yerusalemu
Maandishi ya kiroho ya Watakatifu Wakarmeli kama vile:
Teresa wa Avila
Yohane wa Msalaba
Teresa wa Lisiuex (wa mtoto Yesu),
Pamoja na Watakatifu wengine Wakarmeli.
Na Katiba za Shirika.
Visivyoandikwa
Maisha ya Bikira Maria
Maisha ya Mtakatifu nabii Elia