Jumuiya inayoishi maisha ya tafakari au taamuli ina tabia ya kuundea ulimwengu unaotuzunguka ili kugundua uwepo wa Mungu katika matukio ya kawaida ya maisha ya kila siku. Lakini zaidi kumwona Yeye katika kaka na dada zetu. Hivyo tunaitwa kutambua fumbo la wale tunaoishi nao. Kimsingi Kanuni yetu inatutaka tuwe ndugu (kaka). Na inatukumbusha kuwa uhusiano katika ya mtu na mtu katika jumuiya unatakiwa uendelezwe mara kwa mara. Utatu Mtakatifu, chanzo na mfano wa wa Kanisa ndiyo chanzo vile vile na mfano wa maisha yetu ya kindugu. Maisha ya kukaa pamoja, kufanya kazi pamoja kusaidiana na kutumikiana. Haya maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu. Mungu anatutaka tufungue mioyo yetu kwa maarifa na upendo wake na wa jirani.