Anatarajia kuanza Falsafa mwaka 2023
Nichukue nafasi hii kwanza kumshukuru Mungu, wazazi wangu, ndugu, jamaa na marafiki wote katika maisha yangu ya hapa duniani.
Mimi Kasiano Didas Sokoni mzaliwa wa Jimbo Katoliki la Sumbawanga, Parokia ya Bikira Maria mpalizwa mbinguni-Nkundi, kigango cha Kantawa, jumuiya ya mtakatifu Yohane mbatizaji. Nilizaliwa mnamo tarehe 08/08/2001 katika familia ya Didas Salvatory Sokoni na Grace Egidius Kisato yenye Watoto kumi na mbili, huku mimi nikiwa mtoto wa tatu. Wazazi wakiwa wanajishughulisha na kazi ya ukulima.
ELIMU
Nikiwa mtoto wa miaka nane baada ya kuzaliwa nilianza kusoma elimu ya shule ya msingi mwaka 2008 hadi 2014 katika shule ya msingi Kantawa iliyopo mkoani Rukwa. Ambapo nilidumu kwa muda wa miaka saba mpaka kuhitimu mwaka 2014 katika shule hiyohiyo ya Kantawa. Kwa nguvu za Mungu nilifanikiwa kufaulu nahivyo kuwa miongoni mwa walichaguliwa kuijiunga na masomo ya elimu ya shule ya upili katika shule ya sekondari ya Kipande mkoani Rukwa. Kutokana nahamu ya Kwenda kusoma katika shule ya seminari ndogo, hivyo sikuweza kujiunga na sekondari niliyokuwa nimechaguliwa bali niliamua kujiunga Seminari ndogo ya Mt.Yohane Paulo ii iliyopo mkoa wa Katavi. Huko kuanzia tarehe 13-01-2014 ndipo nilipo fika kwaajili ya kozi fupi yaani pre- form one, kozi iliyodumu kwa muda awa mwaka mmoja. Mwaka mmoja baadae nilianza masomo rasmi ya sekondari 2016-2019 mpaka kuhitimu kidato cha nne katika seminari hiyohiyo. Napo Mungu hakuniacha. Hivyo nilifaulu kujiunga na masomo ya kidato cha tano.
Baada ya kuwa nimefaulu nilichaguliwa kujiunga na shule ya Nkasi High School iliyopo mkoani Rukwa 2020-2022. Napo nilifaulu kuendelea na masomo ya elimu ya juu yaani masomo ya chuo kikuu, lakini kutokana na kuwa nilipenda kuishi maisha ya wakfu, hivyo niliomba kujiunga na Shirika la Ndugu wa Bikira Maria wa mlima Karmeli lenye amakao makuu yake Bunju-Dar-es salaam 2022. Ombilangu lilifanikiwa kukubaliwa na hatimaye kujiunga na malezi hayo ya maisha ya wakfu 18-08-2022 Bunju.
WITO
Wito ni Zawadi yake Mungu mwenyewe amjariaye mwanadamu ili kumtumikia kwa namna ya pekee sana. Safari ya wito wangu ya kutaka kumtumikia Mungu ilianza nikiwa shule ya msingi,na hii ilitokana na baada ya mjomba wangu kupata daraja takatifu ya upadre mwaka 2013 nikiwa dalasa la sita. Tangu hiyo hamu kuniijia niliweza kuwaeleza wazazi wangu tamanio la hamu ya moyo yangu, wazazi wangu waliridhia ombi hilo. Hivyo baada ya kuridhia ndipo walipo amua kunitafutia seminari ndogo kwaajili ya malezi hayo na hatimaye walifanikiwa kupata seminari ya Mt. Yohane Paulo ii iliyopo mkoa wa Katavi. Huko nilisoma miaka mitano (2015-2019) maisha ya huko yalinivutia kwasababau yalikuwa ni maisha kumuweka mtu karibu na Mungu kwa kufundishwa kumjua Mungu na namna ya kuishi ili kuwa karibu naye kwa njia ya Sala na elimu nzuri juu ya Mungu. Malezi hayo yalinifanya kuendelea kuongeza tamanio na tamaa ya kuwa padre.
Nikiwa advance nilikutana na mtu mwenye elimu juu ya upadre yaani upadre wa mashirika, na na wajimbo, aliweza kuelezea na kufafanua kwa undani juu ya upadre wa jimbo na wa shirika. Baada ya kutoa elimu hiyo juu ya upadre na mashirika ,nilijikuta nimevutiwa na na upadre wa shirika hasa shirika la wakarmeli kutokana na karama zake za Sala,Tafakari na Maisha ya huduma kwa watu. Nilimfuata mkufunzi huyo na kumwelezea juu yangu na hivyo aliweza kutafuta namba za mkurugenzi wa miito ili kuongea naye,nilifanikiwa kufanya hivyo tangu nikiwa kidato cha tano 2021. Mkurugenzi baada ya kuongea naye aliweza kukubali na hatimaye kunipa nini chakufanya kwa wakati huo hasa maelekezo juu ya maisha ya Shirika. Baada ya kuhitiomu kidato cha tato na sita (2020-2022), nilipewa tarehe ya kufika katika nyumba ya malezi ambapo mnamo tarehe 18/08/2022 ndipo nilipofika kituoni hapo Bunju. Hapo nilikaa mwaka mmoja 2022-2023.
Mwaka mmoja baadae nilianza masomo Falsafa katika chuo kikuu shirika cha Jordani kilichopo mkowa wa Morogoro. Elimu hiyo ya Falsafa inadu mu kwa muda wa miaka mitatu (2023-2026) sasa ninamalizia mwaka wa tatu wa Falsaf ana pia kujiandaa ya hatua ya kwenda novisiate (novitiate) kwa muda wa mwaka mmoja 2026-2027 inchini Zimbabwe.
Bikira Maria wa Mlima Karmeli ,,,,,,,,,,, utuombee daima.