TUKIO LA NADHILI ZA KWANZA LA MAFRATEL WATATU KATIKA SHIRIKA LA BIKIRA MARIA WA MLIMA KARMELI.
Mnamo tarehe 28/07/2019 saa kumi na moja jioni wanovisi watatu ambao ni Athanas Mhina Ngassa N’O.Carm ,Paschal Dominic Mkaka N’O.Carm Na Dickson Richard Sambala N’O.Carms pamoja na mlezi wa wanovisi Padre Wiseman Msemwa O.Carm waliwasili nchini Tanzania katika uwanja wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakitokea nchini Zimbabwe walipokua wanafanyia malezi ya unovisi. Walipokelewa na padre Victor Maria Alphonce Biramata O.Carm ambae ni mwakilishi wa mkuu wa shirika na mlezi wa waseminari baada ya kuwapokea wanovisi pamoja na mlezi wao kuelekea Parokia ya Bunju kwa ajili ya kupata chakula cha usiku. Na saa mbili usiku waliwasili Parokia ya Bunju na kupokelewa na Mapadri wakarmeli pamoja na Waseminari waliokuwepo Bunju. Baada ya chakula cha usiku wanovisi walipelekwa na Padri Victor Boko kwa Masister Wakarmeli kwa ajili ya kupumzika mpaka siku ya nadhiri .
Tarehe 3/8/2019 kulikua na tukio kubwa na la kihistoria katika shirika na Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli. Siku hiyo Mafrateli watatu waliweka nadhiri zao za muda katika shirika la Bikira Maria wa Mlima Karmeli na vijana hao ni Frt. Dickson Maria Richard Sambala O.Carm, Frt. Athanas Maria Mhina Ngassa O.Carm na Paschal Maria Dominic Mkaka O.Carm . Mafrateli watatu hao ni vijana wa kwanza kuweka nadhiri za Muda nchini Tanzania katika shirika la Bikira Maria wa Mlima Karmeli baada ya watangulizi wao ambao sasa ni Mapadri waliofanyia malezi Napoli Italia na kufunga nadhiri zao za muda na za daima huko.
Tukio zima litanguliwa na adhimisho la Misa Takatifu iliyoadhimishwa na Mwadhama Polcarp Kadinali Pengo, Askofu wa jimbo kuu la Dar –es-Salaam na walio Shiriki Misa Takatifu ni Mapadri wote wakarmeli walioko Tanzania ambao ni Pd. Thomas Mtey O.Carm, Pd. Dominic Somola O.Carm, Pd. Paul Malewa O.Carm, Pd. Paschal Shirima O.Carm ,Pd Victor Biramata O.Carm wageni waliofika katika sherehe ya nadhiri za muda Mkuu wa shirika Zimbabwe Pd. Vitalis Benza O.Carm ,mlezi wa wanovisi kutoka Zimbabwe Pd. Wiseman Msemwa O.Carm, Pd. Denis Omae O.Carm kutoka Kenya ,Pd. Januaris O.Carm kutoka Kenya, Pd. Deodatus Mwageni kutoka shirika la Adorine , mapadri wadekania ya mtakatifu Gasper del bufaro. Mafrateli na masister wakarmeli kutoka kutoka boko mapinga na changombe, watawa wa kike na wa kiume walioalikwa kutoka mashirika mbalimbali, Wazazi jamaa na marafiki wa mafrateli waliweka nadhiri siku hiyo. Katika adhimisho la misa takatifu Baba Mwadhama Kardnali Pengo aliwasisitiza mafrateli wanaoweka nadhiri wawe wasikivu ili waweze kuisikiliza sauti ya Mungu vizuri, hasa katika ulimwengu waleo wenye sauti nyingi ambazo zinaitaji usikivu mkubwa wa sauti ya Mungu. Baada ya homilia yalifuta mahojiano ya vijana wanaoweka nadhiri na mwadhama Policarp Kardinali Pengo, Sbaada ya mahojiano vijana waliweka nadhiri za muda zilizopokelewa na Padri Victor Maria Alphonce Biramata O.Carm ambae ni mwakilishi wa mkuu wa shirika . Baada ya kuweka nadhiri ibada ya misa takatifu iliendelea na baada ya misa takatifu kulikua na tukio la kupiga picha ya pamoja, baina ya mafrateli walioweka nadhiri na mwadhama Kardinali Pengo pamoja na mapadri waliokuwepo kwenye adhimisho la Misa Takatifu.
Baada ya Misa Takatifu kulikua na tafrija fupi iliondaliwa kwa ajili ya kuwapongeza mafrateli walioweka nadhiri ilioanza saa sita na nusu mpaka saa kumi na moja jioni.