Wito ni sauti (vox) anayoisikia mtu ndani ya nafsi yake ikimwita na kumwalika kuishi aina fulani ya maisha. Sauti hii hutoka kwa Mungu mwenyewe. Wito wa kitawa ni neema ya pekee wanayopewa baadhi ya watu ndani ya Kanisa wanaoitwa kuishi maisha ya mashauri ya kiinjili.
1. Wito wa maisha -Kuitwa katika maisha ya ndoa, ya upadre, ya utawa au ya peke yako
2. Wito wa kazi -kwa mfano kuwa mwalimu, daktari, nesi, au polisi.
Watu huwa wanachanganya wanaposema kuwa wito wa upadre au utawa ni kama wito mwingine ule kama vile udaktari, au ualimu. Hilo si sahihi. Wito wa utawa au upadre ni wito wa maisha. Ndiyo maana hata watawa wana wito wa kazi nyinginezo kama vile udaktari, ualimu na kadhalika.
Wote hawa wanaitikia wito mmoja wa utakatifu. Wote tuna wito mmoja wa kuwa watakatifu. Kila mtu huitikia wito huo kwa njia yake aliyopewa na Mungu. Ndipo hapo wengine wanakuwa wanandoa, wengine wanakuwa mapadre, wengine wanakuwa watawa, wengine wanabaki bila kuoa au kuolewa na si watawa wala mapadre (single).
Vijana walioko malezi wakiwa katika sala. Shirika linawapokea vijana wanaotaka kuwa watawa na kumtumikia Mungu katika Shirika la Karmeli. Kijana awe amemaliza kidato cha sita na awe amefaulu. Mpaka sasa kuna vijana wanne ambao wanafanya uzoefu wa kujiunga na shirika la wakarmeli.
Dickson Sambala Kuzaliwa 18.9.1981. High School –Mbezi Beach 2014.
Kuingia malezi - experience 22.7.2014.
Athanas NgasaKuzaliwa 4.7.1992. High school –Kigoma Sch -2014.
Kuingia malezi -experience –17.7.2014.
Pascal Dominic
Kuzaliwa 12.4.1993 High School –Mpwapwa 2014.
Kuingia malezi -experience -21.7.2014.
Deogratias Peter Olomy
Kuzaliwa 18.4.1991. High School -Jitegemee 2011.
Shahada ya kwanza IFM 2014.
Kuingia malezi -experience -
Vijana walioko malezi bunju