Kisakramenti ni kitu chochote kilichotengwa na Kanisa na kubarikiwa na Kanisa ili kiweze kuleta mawazo mazuri na sahihi ya imani na kuongeza moyo wa ibada. Visakramenti viliwekwa na Kanisa Katoliki kwa mfano wa Sakramenti. Lengo ni kuleta matunda ya kiroho, kwa maombi ya Kanisa. Visakramenti vinatakatifuza:
Huduma za Kanisa.
Maisha
Mazingira
na vitu vinavyomfaa mwanadamu.
Visakramenti daima vinaambana na sala na ishara -kwa mfano kuwekewa mikono, ishara ya msalaba na mnyunyizo wa maji.
Visakramenti hutokana na ukuhani wa ubatizo -kila mtu ameitwa kuwa "baraka" na kubariki. Utasikia watu wanasema Mungu akubariki. Wazazi huwabariki watoto.
Kuwa baraka na kubariki
Visakramenti havitoi neema ya Roho Mtakatifu. Ila vinatuandaa kuipokea neema na kisha kushirikiana nayo.
Hakuna kitu chochote ambacho kikitumika vizuri kinashindwa kumwandaa mtu kupata neema.
Visakrameti katika Maandiko Matakatifu
Musa na fimbo ya Aroni.
Fimbo ya Musa inaweza kuchukuliwa kama kisakramenti.
Musa alitumia fimbo aliyooneshwa na Mungu kufanya maajabu na kusaidia Taifa Teule la Israeli kutoka utumwani Misri (Kut 4:17). Kuvuka bahari ya shamu (Kut 14:15-16).
Fimbo ya Aroni inahifadhiwa katika sanduku la agano (Ebr 9:4). Kwa habari zaidi soma Kitabu cha Kutoka sura ya 17.
Hivyo visakramenti vinapewa nguvu fulani ya kumiujiza.
Maana ya baraka
Kubariki ni tendo la kimungu lenye kutoa uzima na Baba ndiye chemchemi. Ni kukutana kwa Mungu na mwanadamu. Mtu anapokea paji la Mungu. Moyo wa mwanadamu waweza kumbariki Yeye nayeubariki.
Ule uzima unakifanya kitu, au mtu awe na nguvu fulani ya kimungu ya kupingana na mwovu.