pichani ni mpostulanti Faustine wakati akijiunga na malezi mwaka 2021
Picha nikiwa naweka sign baada ya kuweka nadhiri za kwanza huko Christe Mambo Zimbabwe.
Picha baada ya misa iliyofanyika siku ya mahafari kuhitimu masomo ya shahada ya Falsafa katika chuo kikuu kishiriki cha Jordan, Morogoro.
HISTORA YA WITO WANGU: FAUSTINE NH’UMBILI
FAUSTINE INNOCENT CEMENT NH’UMBILI ni mtoto wa pili katika famiia ya watoto sita. Nilizaliwa wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza tarehe 15/05/1998. ‘Neno moja nimelitaka kwa BWANA, nalo ndilo nitakalo litafuta, nikae nyumbani mwa BWANA siku zote za maisha yangu. Niutazame uzuli wa BWANA, na kutafakari hekaluni mwake’ ZABURI27;4. Nikiwa na umri wa miaka 2 familia yangu ilipata pigo la kuondokewa na mama yetu mzazi Namshukuru MUNGU, baba yetu alitulea vyema katika malezi ya Imani katoliki ijapo kuwa kwa malezi ya mzazi mmoja.Mwaka 2005 nilijiunga na elimu ya msingi katika shule ya msingi Nyampulukano. Nakumbuka mwaka huo pia baba yetu alifunga tena ndoa jambo lililosaidia kupata tena malezi bora ya wazazi wawili.
Chembechembe za wito wangu zilianza kuonekana nikiwa darasa la pili mwaka 2006 nikiwa mna umri wa miaka 8 . Siku moja tulikwenda kanisani , namna padre alivyokuwa akiongoza ibada ya misa kulinivutia sana. Nikaweka nia ya kuwa padre. Lakini pia nilipotoka nje baada ya misa , nilikuta mazoezi ya watumikaji yakiendelea nilivutiwa sana ,siku hyo hiyo nikajiunga na utumikiaji. Nikiamini nitakuwa nimeanza kuikaribia ndoto yangu. Nilipofika darasa la tano nilijiunga na mafundisho ya ya wito (kawaida jimbo la Geita huwa na mafundisho haya kwa ajili ya maandalizi wanaojiunga na seminari ndogo). Mwaka 2011 nilihitimu darasa la 7 .
Nilipata bahati ya kujiunga na seminari ndogo ya mtakatifu Gregory mkuu iliyopo Sayusayu wilaya Maswa mkoa wa Simiyu katika jimbo katoriki la shinyanga. Mwaka 2012 yaani (pre form one) kwa mwaka mzima.Baadaye mwaka 2013 nilichaguliwa kujiunga na seminari ya mtakatifu Maria Nyegezi iliyopo jimbo katoliki la Mwanza. Nilipofika kidato cha tatu nilipata changamoto katika maisha yangu ya wito na shule . Napena kukiri kuwa kutokna na mkumbo wa vijana lakini pia Dunia kubadilika , vijana wengi tuliamini kuwa masomo ya sayansi ndio mkombozi wa maisha yetu. Licha ya kuwa na wito lakini tuliamin kusoma masomo ya sayansi kungesaidia maisha yetu hapo baadaye. Kulingana na matakwa ya seminari iliwataka wanafunzi wote walio chini ya vigezo vya kusoma masomo hayo kuyaacha mara moja . Hii ilipelekea waseminari wengi kuomba kuhama shule, ili wapate kusoma masomo hayo . Hii ilitokana na ukweli kwamba kwa Tanzania ajira zimekuwa ngumu kwa watu ambao hawakusoma masomo ya sayansi.
Mimi mwenyewe nilijikuta nikipitia katika wimbi hilo ambapo niliamua kuhama shule . Jambo hilo liliathili san asana wito wangu ,nilifikili kuwa sitaweza tena kuwa padre . kutokana na changamoto za ujana sikuwa na tamani tena kuwa padre, lakini kadili nilivyojiweka mbali na mambo ya MUNGU ndivyo yeye alivyojaribu kunisogeza karibu. Mfano;mwaka 2016 nilipohamia shule ya wavulana Musabe sikutamani kujihusisha na jambo lolote la kikanisa lakini ajabu ni kuwa nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa wanafunzi wakatoliki. Hivyo ilinibidi kuwajibika, ukweli ni kwamba hali ya kiroho ilikuwa mbaya pale shuleni , jambo lilifanya niumie nafsi yangu hivyo nilijibidisha kuwafanya wanafunzi kujumuika pamoja . Namshukuru MUNGU wakati wa uongozi wangu tulifanikiwa kufungua tawi la TYCS , ambalo kimsingi lilikuwa halijafunguliwa.
Nilihitimu kidato cha nne mwaka 2017 katika shule ya wavulana Musabe na kupata ufaulu wa daraja la pili (div 2 of 18). Nilichaguliwakujiunga na kidato cha tano katika shule ya sekondari tarakea wilayani Rombo Kilimanjaro .Huko nako nilichaguliwa kuwakiongozi wa TYCS kama mwakilishi wa vikarieti ya Rombo katika uongozi wa jimbo la Moshi. Pia nilipata fulsa ya kuhudhuria mkutano wa taifa uliofanyika TEC Dar es salam nikiwakilisha jimbo la Moshi Nilihitimu kidato cha sita mwaka 2020 na kufaulu kwa daraja la tatu (div 3 of 13) kwa mchepuo wa CBG .Nakumbuka nikiwa kidato cha tano nilianza tena kusikia hamu moyoni mwangu ya kuwa padre. Lakini pia mara nyingi sana nimekuwa nikipata ndoto za kuwa nikihubiri madhabahuni.
Usiku mmoja nikiwa Moshi niliota ndoto. Kuwanilikuwa nimekaa chumbani taa zikiwa zimezimwa,ghaflanilishangaa kuona mwanga mkalisana ndani ya chumba chote . Nikageuka nikaona mtu kavaa mavazi meupe anayeng’aa sana akaniambia ‘ mimi ni YESU , umekuwa ukiomba kuhusu kukua kiroho hivyo inakupasa kuomba kwa kumaanisha sana . Pia usome neno soma ISAYA 6:7-8 kisha akatoweka ISAYA6:7-8 ‘Akanigusa kinywa kinywa changu kwa kaa hilo ,akaniambia .Tazama,hili limekugusa midomo yako ,na uovu wako umeondolewa na dhambi yako imefunikwa. Kisha nikasikia sauti ya BWANA , akasema ‘ tumtume nani atakaekwenda kwa ajili yetu? ‘ Ndipo niliposema ,;nmimi hapa nitume mimi’
Ndoto hiyo ilinifanya niamini kuwa ni kweli usiopingika kuwa BWANA ameniita kwa kazi yake . kuna mambo mengi nisingeweza kuyaeleza yote kwa maandishi. Shirika la wakarmeli nililifahamu kupitia dada yake nafr Victor A. Biramata O.Carm ambaye anaishi Moshi mjini ,alinipa mawasiliano na fr Victor . Namshukuru sana fr Victor kwani alinipa msaada mkubwa sana mpaka kujiunga na shirika hili la wakarmeli Ni mambo mengi sanayaliyotukia na yanayotukia katika katika safari yangu ya wito mengine siwezi kuyaelezea kwa maandishi lakini itoshe kwa haya. Nimalizie kwa kumshukuru MUNGU aliyeniumba na kuniita
‘Bwana akanijibu, akasema ,’Iandike njozi ukaifanye iwe wazi sana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji . Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa,inafanya haraka ili kuufikia mwisho wake, wala haitasema uongo; Ijapokawia, ingoje, kwa kuwa haina budi kuja, haitakawia. HABAKUKI 2;2-3
Mwaka 2021 ndipo nilipoanza masomo yangu ya shahada ya falsafa katika chuo kikuu kishiriki cha Jordan mjini Morogoro. Ambopo kwa neema ya Mungu mimi na wenzangu tulihitimu masomo ya falsafa mwaka 2024. Japo mahafari yetu tulifanya mwaka 2025 baada ya kumalizamwaka wa kikanisa wa unovisi.
Mwaka huo huo wa 2024 tarehe 5 ya mwezi wa 7 ndipo siku tulipo pokelewa katika nyumba ya unovisi ya mtakatifu nabii Eliya, Nyazura . Ilikuwa ni furaha kubwa kwetu mimi pamoja na ndugu zangu Ansbert na John. Na mnamo tarehe 28/06/2025 siku ya jumamosi katika kumbukumbu ya moyo safi wa Bikira Maria tuliweka nadhiri zetu za kwanza na ndipo nikanza kuitwa Br Faustine Maria.
Pia Mwaka huu wa 2025 nilianza masomo ya shahada ya Theology (Taari Mungu) ikiwa ni vigezo vya kila mseminari anaeandaliwa kuwa Padri anapaswa kusoma masomo ya falsafa na theology. Kwangu ni fulsa ya kipekee kuitwa na kumtumikia Mungu katika nafasi hii ambayo Mungu amenipa ndani ya shirika la ndugu wa mama Bikira Maria wa mlima Karmeli.