Bwana Mungu wetu, Mtawala wa enzi, Mwenyezi, Mwenye uwezo, Wewe unayefanya yote na yote unayabadilisha kwa mapenzi yako tu. Wewe ambaye babeli ulibadilisha moto wa tanuru kuwa umande na kuwaokoa watakatifu wako. Wewe uliye mganga wa roho zetu, Wewe uliye wokovu wa wale wanaokukimbilia, tunakuomba na kukusihi, vunja, ondosha na fukuzia mbali, kila aina ya nguvu ya mwovu, kila aina ya uwepo wa utendaji wa shetani, ushawishi wa mwovu, na mabaya yote, uchawi, na nia mbaya za watu na jicho baya la watu waovu linalomlenga mtumishi wako.....
Badilisha adhari za wivu na uchawi kuwa wingi wa nguvu, baraka, mafanikio na upendo.
Bwana unayewapenda watu, nyosha mkono wako wenye nguvu, na viganja vyako nyenye nguvu, njoo kwa msaada na tembelea mtumishi wako huyu, tuma malaika wako wa amani, nguvu na mlinzi wa roho zetu na wa mwili, atakayefukuzia mbali mwovu na nguvu na mabaya na sumu na uchawi wa watu. Bwana ndiye mlinzi wangu ni mwogope nani?
Bwana uwe na huruma na sura yako, okoa mtumishi wako. Bikira Maria atuombee. Amina.